August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Mkuu amhenyesha DC Dodoma

Spread the love

CHRISTINA Mdeme, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma (DC), bado anaumiza kichwa juu ya namna ya kuwahamisha wananchi wanaoishi katika maeneo ya vyanzo vya maji vya Mzakwe, eneo la makutupola Mkoa wa Dodoma, ikiwa ni agizo la Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, anaandika Dany Tibason.

Majaliwa alitoa agizo hilo wakati akifanya ziara yake ya kutembelea vyanzo vya maji katika eneo la Mzakwe bonde la makutupola na kumuagiza DC huyo kuhakikisha wavamizi wote katika eneo hilo wanaondolewa.

Akizungumzia utekelezaji wa agizo hilo, Mndeme amesema kuwa bado hajui ni wapi watapelekwa wakazi watakaohamishwa katika maeneo ya vyanzo vya maji.

“Kwa sasa tunafanya uhakiki wa kutaka kujua ni watu wangapi wanaishi katika vyanzo vya maji. Watapelekwa wapi na kwa utaratibu upi bado hatujajua mpaka muda huu,” amesema.

Mdeme amesema kuwa hatua ya kwanza ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, ni kuundwa kwa kamati ya wataalam mbalimbali wakiwemo wale wa mazingira, ardhi, maji, wahandisi pamoja na wataalamu kutoka Bonde la Ruvu one.

“Tunaendelea kuweka vidhibiti moto katika maeneo mbalimbali ya vyanzo vya maji.

Kwa hatua ya kwanza, tumeanza kuunda kamati ya wataalam mbalimbali kwa ajili ya kushughulikia agizo la Waziri Mkuu la kuwaondoa watu ambao wamevamia katika vyanzo vya maji.

error: Content is protected !!