August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri mkuu akubali yaishe, kujiuzulu leo

Boris Johnson

Spread the love

 

WAZIIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson anatarajiwa kujiuzulu kama kiongozi wa chama tawala cha Conservative baadaye leo, lakini ataendelea kuhudumu kama waziri hadi Oktoba mwaka huu.

Hatua hiyo imekuja baada ya wabunge 50 kujiuzulu kuendelea kuhudumia Serikali anayoiongoza katika kipindi cha saa 48 zilizopita. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa Shirika la habari Uingereza -BBC Kiongozi mpya wa chama cha Conservative anatarajiwa kuchaguliwa na kuanza kuhudumu kama waziri mkuu kufikia mwisho wa mwezi Oktoba.

Hatua hii inajiri siku moja baada ya Johnson kusisitiza kuwa hatajiuzulu kutokana na tuhuma ambazo zimekuwa zikimuandama.

Johnson alikuwa amewaeleza wabunge kwamba ataendelea kutekeleza majukumu yake, licha ya shinikizo la kumtaka ajiuzulu, kufutia kuongezeka kwa idadi ya mawaziri wanaojiuzulu na maofisa wengine wa serikali wanaomtuhumu Johnson kwa kutochuku hatua dhidi ya maofisa wa serikali yake wanaotuhumiwa kuhusika katika unyanyasaji wa kingono

error: Content is protected !!