July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Mkuu ajiuzulu, Rais amgomea

Waziri Mkuu wa Ufaransa, Elisabeth Borne

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Ufaransa, Elisabeth Borne amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Emmanuel Macron ambaye naye amepinga uamuzi huo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya upande wa Rais Macron kushindwa kupata kura nyingi katika uchaguzi wa wawakilishi wa viti vya Bunge.

Hilo ni pigo kwake katika utawala wake ambapo amerejea madarakani hivi karibuni kuendelea na muhula wa pili.

Macron na washirika wake hawatapata Wabunge wa kutosha wanaohitajika kudhibiti Bunge, Mawaziri na hivyo atalazimika kushirikiana na vyama vingine ili kuingoza nchi.

Kutokana na hali hiyo, Rais Macron anatarajiwa kufanya mazungumzo ya kisiasa kuhusu kushirikiana na vyama vingine ili kuingoza nchi.

Ikulu ya Elysée imebainisha kuwa kabla ya mfululizo wa mikutano na viongozi wa vyama vya siasa leo tarehe 21 Juni, 2022, Waziri Mkuu huyo atakutana kwa mazungumzo na serikali nzima mapema alasiri katika ofisi yake Matignon.

Viongozi sita wa kisiasa watapokelewa leo na Rais Macron kutafuta suluhu zinazoweza kujenga siasa za nchi hiyo.

error: Content is protected !!