Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Waziri Mkenda aionya Bodi ya Mikopo ‘nitakula kichwa cha mtu’
Elimu

Waziri Mkenda aionya Bodi ya Mikopo ‘nitakula kichwa cha mtu’

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda
Spread the love

 

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda ametuma salamu kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kwamba ‘atakula kichwa cha mtu’ kutokana na kitendo cha bodi hiyo kushawishi Kamati aliyoiunda kuchunguza utoaji wa mikopo hiyo, ili isitekeleza majukumu yake.

Onyo hilo limekuja baada ya kamati hiyo aliyoitangaza tarehe 31 Julai mwaka huu kushindwa kutekeleza majukumu aliyoipatia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kamati hiyo ilipewa jukumu la kuchunguza uhalali katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2017/2018 mpaka 2021/2022 ili kubaini kama kulikuwa na upendeleo kwa watu wasiokuwa na sifa.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo tarehe 25 Oktoba, 2022 Prof. Mkenda amesema kumekuwa na kusuasua kwenye bodi ya mikopo katika utekelezaji wa kazi hiyo.

“Mara wapite huku mara watokee huku! uchunguzi huu nilisema ufanyike kwa miaka mitano. Lengo lake tungependa kile kidogo tulichonacho kitolewe kwa haki kusaidia wale wenye mahitaji makubwa zaidi.

“Lakini pia kuhakikisha kwamba hakuna fursa ya mimi waziri… mtoto wangu au ndugu zangu wenye uwezo kuhakikisha wao wanapata kwa sababu wao wana connection wakati mtu ambaye hana connection hapati,” amesema.

Amesema kamati hiyo imechelewa chelewa na bodi ya mikopo ina ‘lobby’ (inashawishi) huku na kule ilihali wakifahamu kwamba kamati ya waziri haisimamishwi kufanya kazi.

“Wasi-lobby na bodi ya mikopo nitawachukulia hatua wakiendelea kufanya lobby-lobby kwa sababu wanataka kutuambia na wenyewe wanataka kuficha mambo. Ile kamati ifanye kazi, taarifa ni yetu tutaifanyia kazi kwa ndani kwa sababu sisi hatulengi kwenda kumuumbua sijui mtoto wa Salum amepata mkopo hapana.

“Sisi tunataka kujisahihisha ili kuhakikiha kwamba kile ambacho serikali imetenga kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi kinaenda kwa mlengwa, sasa ninataka kutoa onyo ya kwamba kwenda kulobby sijui eti waziri asimamishe kamati isifanye kazi… hiyo lobbying inaonesha kuna madudu,” amesema.

Ameongeza kuwa akiona hali hiyo inaendelea hatosita kuchukua hatua kali dhidi yao.

“Natuma salamu kwa bodi ya mikopo kwa sababu niliona wamejaribu wanasema ooh tumeitwa sijui tumetuma tusimamishe wakati kazi nimeitoa mimi na mimi ndio nimepewa kazi ya kusimamia mikopo.

“Bungeni watu wanalalamika sana, wanasema kuna yatima hawapewi mikopo, alafu watu wenye uwezo wanapewa mikopo, mimi naunda kamati alafu nisikie kuna ana mtu anasema waziri asiunde kamati, aah! Nitakula kichwa cha mtu,” alionya.

Kamati hiyo aliyoitangaza Waziri Mkenda,inaongozwa na Profesa Allan Mushi ambaye ni mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro, Idd Makame kutoka Zanzibar na Dk. Martin Chegeni ambao wote kwa pamoja ni wataalamu wa mifumo waliobobea katika sayansi ya kompyuta na takwimu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

error: Content is protected !!