May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Mchengerwa atoa maagizo sakata la Steve Nyerere, wasanii

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania, Mohamed Mchengerwa

Spread the love

 

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania, Mohamed Mchengerwa ameingilia kati sakata linaloendelea la msemaji mpya wa Shiriko la Muziki Tanzania, Steve Nyerere na kutaka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kulishughulikia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema hayo leo Jumanne, tarehe 22 Machi 2022 alipozungumza na MwanaHALISI Online kuhusu sakata hilo ambalo limewagawa wasanii wa muziki katika makundi mawili.

Kundi la kwanza wanampinga Steve kuwa msemaji wao na wengine wakitaka aendelee na nafasi hiyo ambayo ameteuliwa hivi karibuni na uongozi wa shirikisho hilo.

Baada ya uteuzi huo na marumbano makali yanayoendelea mitandaoni na Steve mwenyewe leo Jumanne kuzungumza na waandishi wa habari akisema, hawezi kuachia ngazi, mtandao huu umemtafuta waziri mwenye dhamana kujua anashughulikiaje sakata hilo.

“Nimemuagiza katibu mkuu, kushughulikia mgogoro uliopo, kuhusu shirikisho, muungano ambao haupo chini ya Serikali, Nimemtaka katibu mkuu wa wizara awaelekeze, BASATA ambao ndio wamelisajili shirikisho hilo na Katiba yao ipo BASATA, kisheria ni regulator,” amesema Waziri Mchengerwa na kuongeza”

“Wawaite viongozi wa shirikisho, kuwasikiliza na kujua hasa tatizo la mgogoro husika na kushauri ipasavyo kama wasimamizi.”

error: Content is protected !!