Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri Masauni kada wa 17 kuchukua fomu CCM Z’bar
Habari za Siasa

Waziri Masauni kada wa 17 kuchukua fomu CCM Z’bar

Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania akichukua fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM
Spread the love

HAMAD Masauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi leo tarehe 22 Juni 2020, amejitokeza kuchukua fomu kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar kugombea urais. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Kada huyo na waziri alijitokeza katika ofisi kuu za CCM zilizopo Kisiwandui mjini Zanzibar.

Masauni anafanya idadi ya makada wa chama hicho waliojitokeza kuomba kuteuliwa visiwani humo kufika 17. Miongoni mwa waliojitokeza mpaka sasa ni Shamsi Vuai Nahodha, Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar; Hussein Ali Mwinyi, Waziri wa Ulinzi.

Wengine ni Balozi Ali Karume, mtoto wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar marehemu Sheikh Abeid Aman Karume: Jecha Salim Jecha, aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Mbwana Bakari Juma, Mbwana Yahya Mwinyi na Omar Sheha Mussa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!