Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Makamba: Tutabana mianya yote, atakayetoa taarifa Sh. 3 mil
Habari Mchanganyiko

Waziri Makamba: Tutabana mianya yote, atakayetoa taarifa Sh. 3 mil

January Makamba, Waziri wa Ofisi ya Makamo wa Rais, Muungano na Mazingira akiwa katika ziara ya zoezi ya upigaji marufuku mifuko ya plastiki
Spread the love

IKIWA leo tarehe 1 Juni 2019 Serikali imeanza utekelezaji wa marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba amesema atakula sahani moja na watakaokiuka marufuku hiyo. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Makamba ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa marufuku hiyo kwenye soko la Kariakoo, Jijini Dar es Salaam.

Amesema serikali itahakikisha inabana kila mianya ya utengenezaji, utumiaji na usambazaji wa mifuko ya plastiki.

“Tutabana kila mahali, kwa kuzingatia misingi ya busara na hekima kuhakikisha kwamba agizo hili linatekelezwa pasipo kudhalilisha utu wa mtu,” amesema Makamba.

Aidha, Makamba ameagiza watendaji wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na viongozi wa Halmashauri za Jiji na Manispaa Tanzania, kufuatilia utekelezwaji wa agizo hilo usiku na mchana.

“Leo tumefanya hamasa, tukitoka hapa hawa wa NEMC na Manispaa wataingia sokoni na magengeni kufuatilia utekelezwaji wa sheria hii, hakuna Jumamosi wala Jumapili na Mkurugenzi wa NEMC, kesho hakuna Jumapili lazima hili jambo lifuatiliwe,” amesema Makamba na kuongeza.

“Kazi ina anza sasa, kuanzia leo, kesho na mwezi mzima ni kazi inayoendelea kuhakikisha kwamba hakuna anayezalisha, kusambaza wala kutumia mifuko ya plastiki. Watumishi wa NEMC na vijana wetu waliosambazwa nchi nzima kazi itaendelea.”

Katika hatua nyingine, Makamba ametangaza dau nono kwa mitaa itakayofanya vizuri katika utekelezaji wa marufuku ya utumiaji mifuko ya plastiki, akisema kwamba mtaa utakaofanya vizuri utapewa fedha taslimu Sh. 3 milioni.

Pia, Makamba amesema kuanzia Mwezi Julai mwaka huu, serikali itaweka utaratibu wa kutoa motisha kwa watu watakaoripoti uvunjifu wa marufuku hiyo tunatoa wito kwa halmashauri zote nchi kwamba kazi hii inaanza kwa nguvu sana.

Alisema mkoa utakaofanya vizuri itapata zawadi, na hapa Dar es Salaam katika kila wilaya, mtaa utakaofanya vizuri kuhakikisha kwamba hakuna mifuko utapata Sh. 3 milioni. Kwa hiyo halmashauri za Dar kazi kwenu, tutapita kusimamia uzingatiaji wa sheria na nani amefanya vizuri.

Makamba amesema huko mbele kuanzia mwezi wa saba tutaweka utaratibu wa motisha kwa wale watakaoripoti hvunjifu wa sheria hii. Kwa mifuko ya plastic tutaweka utaratibu ule, kuhakikisha wananchi wanachangia utekelezaji wa sheria hii.

Waziri huyo amewahakikishia Watanzania kwamba serikali inaendelea na jitihada za kutatua changamoto zilizopo ikiwemo bei za mifuko mbadala kuwa ghali, akisema kwamba viwanda vya utengenezaji mifuko hiyo vinafanya kazi ya uzalishaji usiku na mchana, pia kuna shehena  ya makontena ya mifuko hiyo inatarajiwa kuingizwa nchini hivi karibuni.

“Serikali ilipoamua kwamba sasa tunapiga marufuku ya plastiki wazalishaji mifuko mbadala walikuwa hawaamini, sababu  huko nyuma tulitangaza na kuahirisha mara tatu, kwa hiyo watengenezaji wa mifuko mbadala wakaona yaleyale,” amesema Makamba na kuongeza.

“Hivi tunavyoongea viwanda vya mifuko hiyo vinazalisha saa 24, kuna makontena yanakuja ya mifuko mbadala, kwa hiyo baada ya mwezi mmoja itafurika mifuko mbadala. Na hali hii itapunguza bei ya mifuko hiyo.”

Akizungumzia kuhusu ziara yake, Makamba amesema amebaini kwamba mwitikio wa wananchi kuacha matumizi ya mifuko ya plastiki unaridhisha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!