July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Majaliwa awakomalia Makamba, Ndalichako

Spread the love

MAJALIWA Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewapa saa 12 wa mawaziri ambao hawajarejesha fomu ya kiapo cha utumishi wa umma, kuzirejesha kwenye Ofisi ya Maadili ya Utumishi wa mma, anaandika Regina Mkonde.

Majaliwa amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam leo, kuhusu maafikiano ya kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika jana juu ya maadili ya utumishi wa umma.

“Kikao tulichokaa jana na Baraza la Mawaziri tulijadiliana juu ya masuala ya maadili ya utumishi wa umma, ndipo tulipoamua kuwasisitiza mawaziri na manaibu waziri wasiorudisha fomu kuzirudisha,” amesema Majaliwa.
Majaliwa ametaja majina ya mawaziri ambao hawajarejesha fomu kuwa ni pamoja na January Makamba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira pamoja na Naibu wake Luhaga Mpina; Charles Kitwanga, Waziri wa Mambo ya Ndani, Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kanda na Kimataifa baada ya kusikia agizo hilo, alirudisha fomu hiyo.
Majaliwa amesema, kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 1995, inawataka watumishi wa umma kurudisha fomu ndani ya siku 30 za utumishi wao baada ya kuteuliwa.
“Sheria ya maadili na utumishi wa umma ya mwaka 1995, inawataka watumishi wa umma kujaza fomu za tamko la rasilimali zao na ya kiapo cha utumishi ndani ya siku 30, atakaye kiuka sheria hiyo, atachukuliwa hatua za kinidhamu,” amesema Majaliwa.
Watumishi wa Umma wanatakiwa kujaza fomu hizo ili kubainisha rasilimali walizonazo kabla ya kuteuliwa kuwa watumishi, na ya kiapo ili kuapa juu ya utendaji kazi uliotukuka katika utumishi wa umma.

error: Content is protected !!