Monday , 27 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Kindamba ‘apigia chapuo’ TTCL kwa SUA
Habari Mchanganyiko

Waziri Kindamba ‘apigia chapuo’ TTCL kwa SUA

Waziri Kindamba, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)
Spread the love

OFISA Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba amewaomba Watanzania kutumia kampuni hiyo kwa mawasiliano kwa kuwa hivi sasa huduma zake zimeboreshwa, anaandika Angel Willium.

Kindamba aliyasema hayo jana wakati wa akitiliana saini makubaliano ya matumizi ya mawasiliano na mtandao wa TTCL na Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kwenye hafla fupi iliyofanyika chuoni hapo.

Amesema licha ya kwamba historia ya kampuni haikuwa njema zamani na kufanya wateja kukosa huduma ipasavyo na hivyo kuamua kuhama lakini kwa sasa hali imebadilika.

“Historia haikuwa njema nyuma kwa TTCL , mtu akipiga simu ilikuwa anapatiwa huduma baada ya wiki mbili hadi tatu, lakini kwa sasa hali imebadilika” alisema Kindamba.

Aidha, Kindamba aliwapongeza SUA kwa kuchukua hatua ya kurejea TTCL kwa mawasiliano na kuahidi kutowaangusha katika utendaji kazi wao na kufanya huduma walizoanza kuzifurahia kuwa endelevu.

Hata hivyo, amesema kuwa TTCL inatarajia kuwa na kasi ya 3G na 4G baada ya wiki moja itakayosaidia kuboresha huduma na kuwezesha upatikanaji wa huduma za TTCL mobile yenye kasi zaidi.

Awali Makamu Mkuu wa Chuo kikuu (SUA) Profesa, Raphael Chipunde amesema kuwa SUA imeamua kuingia mkataba na TTCL baada ya kubaini mabadiliko makubwa yaliyopo kwa TTCL kwa sasa juu ya utoaji wa huduma zao.

Amesema walifikia makubaliano na kuandaa mkataba ambao utaweka chuo katika huduma nzuri itakayowezesha chuo kuendelea kufanya kazi bila matatizo.

“Naweza kusema kwamba Intanet ndiyo imeshika damu kwenye mwili wa binadamu kwa sasa, hivyo bila Intanet ya uhakika chuo kitayumba” amesema,” amesema Profesa Chipunda.

Aidha, amesema kuwa wameamua kuweka makubaliano hayo licha ya kuwa ni ya sehemu ya SUA huku wakiendelea kutumia kampuni nyingine ambayo hakutaka kuitaja na kwamba wakiona TTCL ipo vizuri watahamia kwa asilimia 100.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

ElimuHabari Mchanganyiko

Rubani mtarajiwa Tusiime awashangaza wazazi

Spread the loveWAZAZI walioshiriki siku ya taaluma na maonyesho ya shule ya...

Habari Mchanganyiko

Wanne wadakwa kwa kusafirisha punda 46 nje ya nchi

Spread the loveJeshi la Polisi kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa...

error: Content is protected !!