Friday , 2 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Waziri Kamwele aagiza mazito Mwanza
Habari Mchanganyiko

Waziri Kamwele aagiza mazito Mwanza

Spread the love

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele amemuagiza mkandarasi wa kampuni ya STX Sekyong LTD inayojenga chelezo la meli mpya katika bandari ya Mwanza Kusini, kuikamilisha kabla ya Agosti mwaka huu. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Chelezo hiyo ambayo ina uzito wa tani 4,000 itatumika kubebea meli kubwa na ya kisasa itakayojengwa kwenye bandari  hiyo.

Chelezo hilo litagharimu kiasi cha TSh. 36 bilioni huku meli mpya hiyo yenye uzito wa tani 3,500 itajengwa kwa gharama ya Tsh. 90 bilioni na inatarajiwa kukamilika kwa kipindi cha miezi 10.

Mhandisi Kamwele alisema mkandarasi wa chelezo hilo anapaswa kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha  ujenzi huo kwa muda uliopangwa kwa kutokana na kushindwa kuleta dhamana yake mapema.

Alisema chelezo hilo ni kubwa katika nchi zinazozunguka ziwa Victoria na kwamba kuna uwezekano hata nchi nyingine zinaweza kuja kujengea  meli zao hapa Mwanza kutokana na ubora wake.

“Huyu anayejenga meli anamsubiri huyu anayejenga chelezo amalize kujenga alafu ndiye yeye aanze kujenga, hivyo naagiza kwamba ahakikishe inapofika mwezi wa nane awe tayari amemaliza.

“Yeye ndiyo mwenye makosa kwa sasa inatakiwa afanye kazi usiku na mchana, alafu nasikia Jumapili anapumzika na Jumamosi anafanya kazi mpaka saa sita mchana anaenda kupumzika haiwezikani afanye kazi muda wote,” alisema Mhandisi Kamwele.

Alisema matarajio ya Serikali ni kuona inapofika Juni mwakani meli hiyo mpya iwe imekamilika na kuanza kutoa huduma zake kwa wakazi wa Mwanza na Bukoba Kagera.

Alisema ukarabati wa meli nyingine ikiwemo za Mv. Victoria ambayo ipo katika asilimia 36 na Mv. Butiama ipo asilimia 27 lengo kubwa ni kuhakikisha meli hizo zinakamilika zote.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema ujenzi wa meli hizo itasaidia ukuaji wa uchumi wa mkoa huo  kutokana na asilimia 90 ya watu wanaofanya kazi bandarini hapo ni kutoka Mwanza.

Afisa Mtendaji mkuu wa Kampuni wa Huduma za Meli (MSCL) Mkoa wa Mwanza, Eric Hamis alisema ifikapo Machi mwakani meli za Mv. Victoria na Mv. Butiama zitakuwa zimekamilika.

Sanjari na hayo, amezungumzia tatizo la muda mrefu la malimbikizo ya mishahara kwa wafanyakazi wa kampuni ya huduma za meli, ambalo kwa sasa limetatuliwa, baada ya serikali kutoa kiasi cha Sh. bilioni 2.1.

Pia alisema Serikali imetoa Sh. bilioni 5.9 kwa ajili ya kulipa mishahara kwa miezi 27 katika kipindi hiki cha ujenzi wa meli na kwamba baada ujenzi huo kukamilika, MSCL inapaswa kujiendesha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

Habari Mchanganyiko

Dk. Gwajima atoa maelekezo kwa maofisa maendeleo nchini

Spread the love  WAZIRI wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto,...

error: Content is protected !!