Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri Kabudi apata ajali
Habari za Siasa

Waziri Kabudi apata ajali

Prof. Palamagamba Kabudi
Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amepata ajali ya gari mkoani Morogoro leo Jumatano tarehe 14 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Akizungumza nje ya Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Mkuu wa Mkoa huo, Loata Sanare amesema, leo walikuwa na ziara wilayani Kilosa na tayari walikwisha kufika lakini baadaye walipata taarifa  Waziri Kabudi amepata ajali.

Kabudi naye alikuwa anakwenda Kilosa ambako yeye ni mbunge mteule wa Jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Madaktari wamemcheki hana tatizo kubwa sana, anahitaji kupumzika. Niwatoe wasiwasi  wana Kilosa na Watanzania, Mzee Kabudi amepata ajali lakini anaendelea vizuri,” amesema.

Sanare amesema, baada ya mapumziko aliyopewa Waziri Kabudi, watapata maelekezo mengine ya nini cha kufanya.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!