Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri Jafo ‘ashikwa shati’
Habari za SiasaTangulizi

Waziri Jafo ‘ashikwa shati’

Spread the love

IMANI kwa Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa (TAMISEMI), imeanza kutoweka. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

“Sisi NLD hatuna imani naye licha ya kuagiza kuwa wagombea wote walioenguliwa, warudishwe, agizo ambalo hana mamlaka nalo kikanuni wala kisheria,” alisema Oscar Makaidi, Mwenyekiti wa Chama cha NLD kwenye taarifa yake jana tarehe 13 Novemba 2019.

NLD kimekuwa chama cha nane kujitoa kwenye uchaguzi huo, ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ndio kilianza kujitoa na kufuatiwa Chama cha ACT-Wazalendo, Chama cha Umma (Chauma), NCCR-Mageuzi, UPDP, Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha Kijamii (CCK).

Makaidi amemtaka Waziri Jafo kujiuzulu mara moja kwa madai, ameshindwa kusimamia uchaguzi huo kama waziri mwenye dhamana na kulitia taifa hasara.

Akizungumza na gazeti mmoja nchini, Shekh Hamisi Mataka ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), ameshauri kuwepo na meza huru ya mazungumzo kuhusu uchaguzi huo.

Amesema, kutokana na sintofahamu hiyo, sasa ni vema suluhu ikapatikana mapema huku akitaka Baraza la Vyama vya Siasa litumike kutafuta suluhu.

Askofu Benson Bagonza wa Dayosisi ya Karagwe ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), ameshauru kuundwa kwa chombo huru kitachosimamia uchaguzi huo tofauti na ilivyo sasa.

Amesisitiza kwamba ili uchaguzi uwe huru na haki, kunahitajika tume huru “Mwaka 2020 ili uchaguzi uwe huru na haki, tunahitaji Tume Huru.”

“Ili uchaguzi mkuu wa 2020 nao uwe wa huru na haki, tunahitaji Tume Huru ya Uchaguzi.

Askofu Bagonza amesema, kwa sasa TAMISEMI na wasimamizi hawawezi kuaminika, na hata kama wakiweza kufanya vizuri, bado hawatoaminika.

“Kinatakiwa kiundwe chombo huru ambacho kitaaminika na vyama vyote,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!