Monday , 26 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri Jafo aanza kazi na tambo
Habari za Siasa

Waziri Jafo aanza kazi na tambo

Selemani Jafo, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Spread the love

WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amewataka watumishi wa Wizara hiyo kujipima na kujitafakari katka utendaji wao wa kazi na wale wanaodhani hawawezi kufanya kazi kwa kasi ya sasa bora wakae pembeni, anaandika Dany Tibason.

Jafo ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akijitambulisha kwa watumishi wa Wizara ya TAMISEMI baada ya kuapishwa kuwa Waziri kamili wa Wizara hiyo.

Amesema kamwe hataweza kuwavumilia watumishi ambao wanafanya kazi kwa mazoea wasiopenda kujali muda na wale ambao hawapendi kuthamini utu wa mtu wakiwa kazini.

Amesema kutokana na hali ya sasa na ukubwa wa Wizara ulivyo kila mtendaji anastahili kufanya kazi kwa kiwango kikubwa ambacho kitakuwa na manufaa kwa serikali na jamii kwa ujumla wake badala ya watu kufanya kazi kwa kiwango kidogo na kwa mazoea.

Mbali na hilo aliwataka watumishi wote kuwa na mipango kazi ambayo inatekelezeka sambamba na kutoa ripoti ya kazi zao iliyo sahihi na siyo ripoti ya kupikwa ambayo inaandikiwa hotelini.

Kutokana na hali hiyo Jafo amewaagiza wakurugenzi wote wa kila idara kuhakikisha wanawapatia mipango kazi watumishi na kuwapima kwa viwango vyao vya kufanya kazi na ikionekana kuna mtumishi ambaye hawezi kufanya kazi kwa viwango vinavyotakiwa ni bora akakaa pembeni.

“Napenda kusema kuwa kwa sasa sitaki kuona mtumishi anafanya kazi kwa mazoea na katibu mkuu nakuagiza tupangiane kazi na kazi hiyo ipimwe kwa viwango vinavyotakiwa ili kazi iweze kuleta tija kwa serikali na kwa jamii.

“Hapa TAMISEMI siyo dampo la kuleta watumishi wa kukaa maofisini badala yake kila mtumishi atoke ofisini na afanye kazi yenye tija na afanye kazi yenye tija kwa serikali na kwa jamii kwa ajili ya maendeleo”amesema Jafo.

Mbali na hayo Jafo amewakemea watumishi ambao badala ya kufanya kazi kwa ufasaha wamekuwa mabingwa wa kupika majungu kwa lengo la kuwagombanisha watumishi.

“Lazima kutambua kuwa TAMISEMI ni chombo kikubwa ambacho kinaweza kusababisha kuwepo kwa maendeleo au nchi kutokuwa na maendeleo hivyo watumishi wanatakiwa kuhakikisha wanafanya kazi na siyo kuwa watumishi washona suti kwa maana ya kukaa maofisini wakizunguka katika viti badala yake kila mmoja afanye kazi kwa kukimbizana na muda,” amesema.

Kuhusu elimu Jafo amesema inasikitisha na kutia aibu kwa shule za serikali za vipaji maalum kutokushika nafasi ya kumi bora katika mitihani ya kitaifa badala yake shule za binafsi ndizo zinafanya vizuri jambo ambalo halikubaliki.

Kutokana na serikali kuhimiza suala la elimu ni lazima shule za serikali za vipaji maalum za serikali kufanya vizuri ili kuondokana na aibu hii.

“Tuna shule 22 za serikali ambazo ni vipaji maalum lakini jambo la ajabu shule hizo hazipo hata kumi bora hapa lazima tujiulize ni kwanini shule hizo zinakuwa nyuma kielimu, sasa lazima tufaanye kila juhudi kuhakikisha shule hizo zinafanya vizuri kushinda shule za binafsi na siyo kwa nguvu yoyote bali kuziwezesha shule hizo kufanya vizuri”alisema Jafo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!