WIZARA ya Afya nchini Tanzania, imetaka wananchi wanaokabiliwa na vitendo vya kikatili kwenye familia/nyumba zao, kuwasiliana na maofisa wa wizara hiyo moja kwa moja kwa kupiga simu ili kupata msaada zaidi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Kwenye tamko lake dhidi ya vitendo vya kikatili kwa wanawake na watoto leo tarehe 29 Januari 2021, Dk. Dorothy Gwajima ambaye ni waziri wa wizara hiyo amesema, namba zitazotumika kupokea malalamiko ama taarifa hizo ni yakwake mwenyewe-0734124119, Naibu Waziri, Dk. Godwin Mollel-0764594078, Katibu Mkuu, Profesa Mabula Mchembe-0739900100 na Kamishna wa Ustawi wa Jamii-0754497122.
Kwenye tamko hilo, Dk. Gwajima amesema, kumekuwa na ongezeko la vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na mauaji na hata wengine kutaka kujiuzulu.
Ameagiza Maofisa wa Ustawi wa Jamii ngazi zote za halamshauri pamoja na mambo mengine, kutenga siku moja katika wiki ili kusikiliza changamoto za kijamii ikiwemo migogoro ya familia.
Soma zaidi tamko lake…
Leave a comment