Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Waziri Bashungwa aipa siku 7 COSOTA
Michezo

Waziri Bashungwa aipa siku 7 COSOTA

Spread the love

 

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania, Innocent Bashungwa ametoa siku saba kuanzia kwa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA), kufanya kikao cha kuwapitisha wadau marekebisho ya Kanuni ya Leseni Utangazaji na Maonesho kwa Umma ya mwaka 2003 ili kupata maoni yao. Anaripoti Anitha Jonas-COSOTA … (endelea).

Bashungwa alitoa agizo hilo jana Jumapili, tarehe 8 Agosti 2021, Jijini Dar es Salaam alipofanya kikao na menejimenti ya taasisi hiyo ya kufuatilia marekebisho ya kanuni hiyo ambayo imefanyiwa marekebisho ya tozo katika maeneo mbalimbali ya biashara yanayotumia kazi za Muziki.

‘’Ndani ya wiki moja kuanzia leo (jana) muende kwa wadau mkawapitishe katika kanuni hizi ili nao watoe maoni yao, hili tunatakiwa kulikamilisha kwa haraka ikumbwe kuna maagizo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano kuwa tunatakiwa kugawa mirabaha mwezi Disemba ni lazima mkamilishe hili kwa haraka,’’alisema Bashungwa.

Aliitaka COSOTA kuhakikisha inazingatia maoni yote ya wadau ili kuepuka migogoro wakati kanuni hizo zitakapoanza kutumika na kwa maeneo hayo niliyowaelekeza kuyafanyia marekebisho mizingatie kwa kuangalia hali ya uchumi na mwenendo wa athari za ugonjwa wa Corona.

Kwa upande wa Mwanasheria wa COSOTA, Lupakisyo Mwambinga katika wasilisho lake la marekebisho ya kanuni hizo alifafanua baadhi ya maeneo yamefanyiwa marekebisho kutokana na kuwa na kanuni hiyo imekuwa yamuda mrefu hivyo gharama zake zimekuwa haziendani na maisha ya sasa.

“Katika marekebisho ya Kanuni hizi tumezingatia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama ikiwa ni pamoja na kushusha gharama chini ya yale mapendekezo ya awali ya wadau hii ni kwa kuzingatia hali ya sasa ya kiuchumi na kuweka mazingira rafiki ya ambayo yataweza kulipika,” alisema Mwambinga.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Emmanuel Ishengoma alisema, katika mapendekezo ya marekebisho hayo, yatasaidia kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mirabaha kwa maeneo ambayo awali yalikuwa hayatozwi gharama hizo za matumizi ya kazi za muziki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!