Monday , 4 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Bashungwa aagiza wahandisi kujengewa uwezo
Habari Mchanganyiko

Waziri Bashungwa aagiza wahandisi kujengewa uwezo

Spread the love

WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) kushirikiana na Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET) kuweka utaratibu endelevu wa kuwajengea uwezo wahandisi ili waweze kuendana na mabadiliko ya teknolojia. Anaripoti Danson Kaijage, Arusha (endelea).

Bashungwa ameagiza hayo jana tarehe 30 Novemba wakati akifungua Kongamano la Kitaifa la 32 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Arusha (AICC).

“Kutokana na asili ya tasnia ya uhandisi, Mhandisi ni mwanafunzi maisha yake yote, ninawaagiza ERB wakiungwa mkono na IET kuweka mpango maalumu wa kuwapatia ujuzi wahandisi wetu walioko kazini kwa kutumia miradi iliyopo” amesema Bashungwa.

Bashungwa ameitaka Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) kupitia upya vigezo vya usajili wa wahandisi kwa kufungua milango na kuondoa vikwazo visivyo vya lazima katika usajili.

“Idadi ya wahandisi mahiri inatakiwa kuwa muhandisi mmoja kati ya wananchi 5,000, kwa hesabu za haraka, tunatakiwa kuwa na wahandisi mahiri zaidi ya 12,000 lakini nimeambiwa wahandisi washauri waelekezi ni chini ya 500”

Aidha, Bashungwa amesema azma ya Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kujenga uchumi ulio imara ndio maana Serikali, imejiegemeza kwa kiwango kikubwa kujenga uwezo, juhudi, maarifa, weledi, nidhamu, umakini na ufanisi kwa wataalam hao.

Bashungwa ameeleza kuwa wahandisi wabobezi wana deni la kuwalea na kuwaongoza wahandisi wachanga ili waweze kuishi ndoto zao.

Kadhalika, Bashungwa ameitaka Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) pamoja na Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET) kushirikiana kwa pamoja kutatua changamoto zinazoikabili tasnia ya uhandisi.

Bashungwa pia amewaagiza Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Bodi ya Makandarasi (CRB), Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) pamoja na Bodi ya Wakadiriaji Majengo (AQRB) kukamilisha mpango wa kushirikisha wataalamu wa ndani kuuwasilisha wizarani mpango kazi wa utekelezaji wa maagizo yote yaliyotolewa katika kikao tulichokaa na masuala ya ujenzi.

Waziri Bashungwa amemwakilisha Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa Majaliwa ambaye alitarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la 32 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania lililokuwa na Maudhui “Ubunifu unaotoa Suluhisho katika Uhandisi kwa Maendeleo Endelevu”.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

TEF yaomboleza kifo cha Mzee Mwinyi

Spread the loveJukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

Maambukizi ya UKIMWI Lindi yapungua

Spread the loveMaambukizi ya Virusi vya UKIMWI yamepungua katika Manispaa ya Mkoa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mgomo kitita kipya cha NHIF: Serikali yaita hopsitali binafsi mezani

Spread the loveSERIKALI imekiita mezani Chama cha Wenye Hospitali Binafsi (APHFTA), ili...

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

error: Content is protected !!