Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri Aweso aipa maagizo 3 Ewura
Habari za Siasa

Waziri Aweso aipa maagizo 3 Ewura

Spread the love

 

WAZIRI wa Maji nchini Tanzania, Jumaa Aweso ameipa maagizo matatu Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) ikiwemo kudhibiti upagwaji wa gharama za maji bila utaratibu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Aweso amesema hayo leo Ijumaa, tarehe 17 Septemba 2021 jijini Dar es Salaam, wakati akizindua Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Dar es Salaam (Dawasa).

Bodi hiyo yenye wajumbe tisa inaongozwa na Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange na Katibu wake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja.

Wakati akizungumza kwenye uzinduzi huo, amempongeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mhandisi Godfrey Chibulunje kwa kuhudhuria shughuli hiyo na kutumia fursa hiyo kumpa maagizo.

Mosi, Aweso amemtaka Chibulunje kuwa “Lazima uendelee kuwa mkali. Mamlaka inatoza bili ambayo haijaidhinishwa na Ewura tuambie.”

Pili, Waziri Aweso ameitaoa Ewura kuchukua hatua dhidi ya “Mamlaka inayobambika bili tuambie tutashughulika naye. Hatutaki wananchi wabambikiwe bili.”

Mwisho, ameitaka Ewura kufanya “tathimini ya gharama ya uunganishaji wa maji majumbani, serikali inaweka fedha nyingi kwenye miradi. Tunataka kukua Kumuunganishia maji mwananchi ni bei gani.”

“Kama ni gharama kupungua ipungue. Kwa hiyo Ewura ifanyieni kazi hii,” amesema Waziri Aweso

Ameitaka bodi hiyo kuisimamia vyema Dawasa ili iweze kuendeleza kazi nzuri ya kuwafikishia wananchi maji hususan wale wa maeneo ya pembezoni.

Ameipongeza Dawasa kwa kazi nzuri na kuwataka kuongeza kasi zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!