Saturday , 2 December 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Waziri atia msisitizo uandishi wa Insha
Elimu

Waziri atia msisitizo uandishi wa Insha

Spread the love

WILLIAM Ole Nasha, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, amewataka wakuu wa shule nchini kushawishi wanafunzi kuchangamkia fursa za mashindano ya uandishi wa Insha za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo 11 Desemba 2019, jijini Dodoma hafla ya kutunuku vyeti kwa washindi wa kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha za SADEC na EAC.

Amesema, uandishi wa Insha za SADEC na EAC utaweza kuwasaidia na kuwaongozea uwezo wanafunzi katika kukuza ujuzi wa lugha.

“Napenda kusisitiza kuwa, wakuu wote wa shule kuendelea kuwashawishi wanafunzi kuchangamkia fursa za mashindano kwani pamoja na kuwaongozea uwezo wao katika kukuza ujuzi wa lugha, uandishi wa insha unaongeza maarifa kwa ujumla,” amesema.

Naibu Waziri huyo aliwataka pia Wakuu hao kusimamia kwa umakini mchakato wa mashindano hayo ili kuhakikisha ushiriki wa wanafunzi wengi.

“Nawaagiza kila Mkuu wa shule kuteua mratibu atakayefanya kazi ya kusimamia wanafunzi ili wazingatie na kufuata taratibu zote za uandishi wa insha ili tuweze insha nzuri na kuziwasilisha katika mashindano ya kanda,”amesema.

Naye,Mratibu wa Shindano hilo,Sylvia Chinguwile alimtangaza, Vanessa Lema kutoka Shule ya Sekondari Longodo Mkoani Arusha  ambaye yupo kidato cha nne kuwa mshindi wa shindano hilo.

Wengine walioshinda katika shindano hilo ni Thomas Kalisha mwanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule ya Kibasila  ya Jijini Dar es salaam ambaye alishika nafasi ya pili,huku nafasi ya tatu ikishikwa na Monica Nyamhanga mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Heritage ya Mkoani Pwani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Janeth Mbene apongeza HKMU, ataka wahitimu wajiajiri

Spread the loveWAHITIMU wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), ...

Elimu

Prof. Mkenda avitaka vyuo vikuu Afrika kujikita katika tafiti

Spread the loveWAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Prof. Adolf...

ElimuTangulizi

Tazama matokeo darasa la saba 2023 hapa

Spread the loveBARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) leo Alhamisi limetangaza matokeo ya...

Elimu

Shule za St Mary’s zang’ara matokeo darasa la saba

Spread the loveSHULE za St Mary’s nchini zimeendelea kufanya vizuri kwenye mitihani...

error: Content is protected !!