Friday , 9 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri ataka bunge limpe tuzo Kikwete
Habari za Siasa

Waziri ataka bunge limpe tuzo Kikwete

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso. Picha ndogo, Ridhiwan Kikwete, Mbunge wa Chalinze
Spread the love

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso amesema kama Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lingekuwa linatoa tuzo, angeshauri litoe kwa Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Aweso ametoa ushauri huo leo tarehe 14 Novemba 2018 bungeni jijini Dodoma mbele ya Naibu Spika Tulia Ackson, akisema kwamba Kikwete amekuwa akitetea masilahi ya wananchi wake na kwamba anastahili kupata tuzo.

“Laiti kama bunge lako lingekuwa linatoa tuzo ningeshauri litoe kwa Kikwete kutokana na kutetea wananchi wake,” amesema Aweso.

Akijibu swali la Kikwete kuhusu kusuasua kwa utekelezwaji wa mradi wa miundombinu ya maji awamu ya tatu Chalinze, Aweso amesema serikali imeamua kumrejesha kwa masharti mkandarasi wa mwanzo wa mradi huo, aliyesimamishwa kutokana na sababu mbalimbali ili aukamilishe mradi huo.

“Serikali inaendelea na uboreshaji huduma ya maji Chalinze kwa sasa serikali inatekeleza awamu ya tatu, serikali imeamua kumrejesha mkandarasi wa mwanzo ili amalize kazi, mkandarasi huyo amepewa masharti mapya ya kuhakikisha unamalizika kwa kasi, anatakiwa kukamilisha Desemba 2018 wizara itaendelea kufuatilia akamilishe kazi, na asipofanya hivyo atachukuliwa hatua,” amesema Aweso.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!