Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri asikia kilio cha Mch. Msigwa
Habari za Siasa

Waziri asikia kilio cha Mch. Msigwa

Waziri wa Nchi Ofisi a Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Ummy Mwalimu
Spread the love

KAULI ya Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwamba, ni marufuku madaktari, wakunga na wauguzi nchini kufukuzwa ama kusimamishwa ovyo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kabla ya kauli ya Ummy, Mch. Peter Msigwa, alimlalamikia waziri huyo kwamba, Ally Hapi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa amekuwa akifanya ziara kuwadhalilisha wataalamu, jambo ambalo limesababisha wataalamu wengi wa afya kukimbia hivyo kuongeza tatizo la huduma ya afya mkoani humo.

Mch. Msigwa alifikisha mashitaka hayo bungeni alipokuwa akichangia hotuba ya wizara hiyo juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/20.

Kutokana na kauli hiyo, Waziri Ummy amesepiga marufuku ya kubughudhi watumishi hao wakati akihitimisha hotuba ya bajeti ya wizara yake tarehe 8 Mei 2019.

Amesema, kama daktari, muuguzi au mkunga amekosea, wapelekwe kwenye mabaraza yao ambayo ndiyo yanashughulikia suala la nidhamu kwa kada hiyo ya wstumishi.

“Kutokana na hali halisi ilivyo, muuguzi mmoja anafanya kazi ambayo ingefanywa na wauguzi watano na madaktari wanafanya kazi hivyo si vema kuwakatisha tamaa.

“Sisi kwa kutambua umuhimu wao tutaendelea kuwatetea wauguzi na madaktari wetu, tusiwakatishe tamaa na isitoshe hao wenye fedha hawaendi kutibiwa kwenye hizo hospitali za Serikali, matokeo yake wanaoumia ni watanzania,” amesema Waziri Ummy.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!