October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri ashangaa madini kulindwa na wageni

Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu)

Spread the love

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira Vijana na wenye Ulemavu, Jenister Mhagama amevishangaa vyombo vya ulinzi na usalama nchini, kuruhusu sekta ya madini kulindwa na wageni, wakati wao wapo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mhagama alisema kuwa ni aibu kwa nchi kuruhusu vyombo vya ulinzi kutoka nje ya nchi kuja kulinda madini wakati polisi na vyombo vingine vipo.

Aidha mhagama amesema kuwa kumekuwepo na kasumba ya vyombo vya ulinzi na usalama kuwasumbua wawekezaki wageni ambao wametimiza vigezo na masharti badala ya kuwalinda.

“Niwatake viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama msiwaonee wawekezaji wa madini kwa kuwakamata kiholela holela na badala yake muwape ushirikiano stahiki wa wawekezaji ambao wanatimiza na kutekeleza sheria na utaratibu wa nchi.

Mhagama alisema wawekezaji hao wakisumbuliwa wanaweza kuondoka hali itakayopelekea Serikali kukosa mapato kutokana na kodi za wawekezaji hao.

Aidha Waziri huyo amewataka viongozi hao kuwalinda wawekezaji hao na kuwapa haki stahiki kwa lengo la uboreshaji huduma za Kijamii nchini.

“Sekta ya madini ni sekta nyeti sana hapa nchini, hivyo yombo vya ulinzi na usalama wakifanya kazi yao kwa kufuata sheria¬† na utaratibu za nchi, Tanzania haitakuwa maskini,” alisema Mhagama.

“Tunawategemea sana viongozi wa Ulinzi na usalama hapa nchini ili kuendelea na pato stahiki la Taifa ambapo lengo ni kufikia asilimia 10 katika kuchangia pato hilo,” alisema.

Mhagama alisema ili viongozi hao waweze kudhibiti rasilimali madini kwa uhakika wanatakiwa wawe na mtandao ufuatiliaji kutoka eneo moja kwenda lingine.

Naye Waziri wa Madini, Dotto Biteko alisema baada marekebisho ya sheria ya Madini Mwaka 2017 ilirahisisha mambo mengi sana, mapato yameongezeka katika latina, dhahabu, almasi na Tanzanite.

Biteko alisema kwa mwaka uliopita serikali ilikusanya kiasi cha Sh. 346 bilioni kutokana na madini, hivyo kama yatasimamiwa vizuri mwaka huu yanaweza kuingiza zaidi ya Sh. 470 bilioni.

error: Content is protected !!