September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waziri aonya watumishi wa umma

Spread the love

SELEMAN Jafo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ametangaza kupambana na watumishi pia watendaji katika halmashauri  ambao hawatimizi wajibu wao, anaandika Dany Tibason.

Katika hatua hiyo amesema, watendaji na watumishi ambao wanajiona kuwa, hawana kasi ya kutimiza wajibu wao kwa viwango ambavyo vinakubalika, ni bora wakajiondoa wenyewe na kuomba kazi nyingine ambayo wataona wanaiweza.

Ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya Chemba mkoani Dodoma.

Amesema, inasikitisha kuona miradi mingi katika halmashauri inatekelezwa kwa kiwango cha chini jambo ambalo linaisababishia serikali hasara.

“Wapo baadhi ya wahandisi ambao wanafanya kazi kwa maslahi yao binafsi badala ya kufanya kazi kwa maslahi ya jamii na taifa kwa ujumla.

“Unaweza kukuta wa ujenzi wa barabara ambao unatakiwa kujengwa kwa mita sita au mita saba lakini mhandisi anafanya ujanja anapunguza mita mbili au mita tatu na kwa kufanya hivyo tayari anakuwa ameishaujumu kiasi kukubwa cha fedha ambazo zinaingia mifukoni mwake” amesema Jafo.

Amesema kuwa, ametembelea halmashauri mbalimbali na kukuta majengo ambayo kabla hayajakabidhiwa, tayari yanakuwa na nyufa bila mtu yoyote kuchukuliwa hatua.

Amesema, watendaji ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea ni bora wakaacha mara moja na kama haiwezekane ni bora wajitumbue kabla hawajatumbuliwa.

Katika hatua nyingine amesema, kumekuwepo kwa uzembe kwa watumishi wengi wa serikali za mitaa kusababisha kuibuka kwa migogoro.

Amesema, watumishi wengi wanakaa ofisini kwa lengo la kusubiri kuletewa taarifa, na wakati mwingine wanaletewa taarifa ambazo hata wao watendaji hawazijui.

 

error: Content is protected !!