Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Waziri anusa ufisadi matumizi fedha za UVIKO-19
Afya

Waziri anusa ufisadi matumizi fedha za UVIKO-19

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini Tanzania, Dk. Godwin Mollel
Spread the love

 

NAIBU Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, ameagiza uchunguzi ufanyike dhidi ya matumizi ya fedha za kukabiliana na athari za Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19), zilizotumika katika ujenzi wa miundominu ya Hospitali ya Rufaa ya Wagonjwa wa Akili Mirembe, akisema kuna viashiria vya ubadhirifu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Dk. Mollel alitoa agizo hilo hivi karibuni alipotembelea Hospitali ya Mirembe, iliyoko jijini Dodoma , kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya miradi inayotekelezwa na Serikali kupitia fedha hizo.

Naibu Waziri huyo wa Afya, alihoji kwa nini hospitali hiyo itumie kiasi cha Sh. 900 milioni kukarabati miundombinu ambayo katika hospitali nyingine imetumia Sh. 350 milioni.

“Unaweza kushangaa unakuta sehemu moja wanafanya ukarabati kwa gharama ya Sh. 350 milioni na sehemu nyingine ukarabati wa aina hiyo hiyo unafikia kiasi cha sh. 900 milion katika eneo hili, hapo najiuliza maswali ni kwa sababu gani? Nahitaji majibu ya kina kuhusiana na maagizo hayo na nitarudi hapa ndani ya miezi mitatu na nisipopata majibu ya kuridhisha hatua nyingine zitafuata,” alisema Dk. Mollel.

Katika hatua nyingine, Dk. Mollel amewataka watumishi wa umma kusimamia fedha za miradi ya maendeleo zinazoletwa na Serikali katika maeneo yao.

“Ni lazima kila mmoja ambaye anatumika katika Serikali hii kusimamia fedha za maendeleo, lazima awe na uchungu wa fedha hizo vinginevyo sheria lazima zifuatwe. Nayaongea haya ili kutuma ujumbe Kwa kila anayepewa dhamana ya kusimamia fedha za Serikali, awe na uchungu wa fedha hizo na kuhakikisha zinafanya kazi yenye tija, maana zingeweza kubaki na kununua dawa, vitenganishi na vifaa tiba,” alisema Dk. Mollel.

Katika hatua nyingine, Dk. Mollel aliipongeza hospitali hiyo kwa kuendelea kutibu wagonjwa licha ya changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.

“Kama muuguzi na daktari wa mirembe wanapokea wagonjwa walioletwa kwa mitutu au pingu halafu, akifika mbele yao anafunguliwa na kuachiwa huru ahudumiwe ni kazi sana. Mirembe wanapokea taarifa za wagonjwa za kutisha tofauti na hosipitali zingine , lengo la ziara ni wizara inataka kuibeba mirembe na watumishi wake tofauti na hosipitali zingine,” alisema Dk. Mollel.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!