August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri amtwisha ‘zigo’ Rc Mongella

Spread the love

MHANDISI Gerson Lwenge, Waziri wa Maji na Umwagiliaji amemtaka John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kufuatilia na kubaini kilichosababisha kukwamisha mradi wa maji wa Kazilankanda uliojengwa chini ya kiwango, anaandika Moses Mseti.

Mradi huo unaotekelezwa katika vijiji 13 vya Wilaya ya Ukerewe mkoani humo, mpaka sasa umegharimu Sh. 4,034,277, 621 na kukamilika kwake utaweza hudumia watu 68,038. Mradi huo unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu.

Kauli hiyo imeitoa leo mara baada ya kukagua mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Ziwa Victoria awamu ya pili (LVWATSAN-II).

Amesema, mradi wa Kazilankanda unaofadhiliwa na Benki ya Dunia umekwama licha ya serikali kupeleka fedha.

“Serikali ilileta fedha kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kutoka kwenye mfuko wa maji lakini zikatumika nje ya maelekezo, mkafanyia jambo lingine na kununulia funiture (samani) za ofisi. Hairuhusiwi fedha hizo zitumike kufanya kazi tofauti.

“Nitafuatilia mradi wa hapa nijue kilichojiri na nimemwagiza mkuu wa mkoa afuatilie pia maana ni ninyi (halmashauri) ndio mlioleta cheti mkatumiwa fedha kwa ajili ya mradi huo mnaoutekeleza,” amesema Lwenge.

Waziri huyo amesema, miradi mingi ya umwagiliaji katika wilayani Ukerewe imejengwa chini ya kiwango na hivyo wataalamu wataletwa ili watafiti upya ili iweze kutekelezwa.

Katika hatua hiyo amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuweka utaratibu wa kuvuna maji ya mvua na halmashauri ijenge mabwawa madogo madogo yasidie kupata maji ya kutosha kwa matumizi mengine na kuendesha kilimo cha umwagiliaji.

Kuhusu halmashauri ya wilaya kukosa wahandisi wa kusimamia miradi amesema, serikali haitaleta waandisi bali wa wilaya na mkoa watalazimika kusimamia kazi hizo na atakayesanifu mradi ndiye atakaye ujenga na kama alikosea itakula kwake.

Estomihn Chang’a, Mkuu wa Wilaya amesema, mradi huo wa Kazilankanda unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu kutegemea fedha zitakazoletwa na serikali kuu ambapo  hadi sasa umegharimu Sh.4,039,277,642.40  na ulikisiwa kugharimu Sh .7,348,516,987 hadi kukamilika.

Amesema kuwa, Septemba 2016 halmshauri ilipeleka madai y ash. 1,418,049,621 wizarani  kwa ajili ya kuwalipa wakandarasi kwa kazi iliyoelekezwa na ili kuharakisha utekelezaji wa mradi huu halmashauri imeugawa katika vipande vitano.

error: Content is protected !!