March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waziri afariki akisaka hela za zahanati

Marehemu Slim Chaker

Spread the love

WAZIRI wa Afya Nchini Tunisia amefariki kutokana na mshutuko wa moyo baada ya kushiriki katika mbio za kuchangisha fedha za kusaidia kupambana na ugonjwa wa saratani.

Slim Chaker, 56, aliugua baada ya kukimbia mita 500 na kufariki kwenye hospitali ya kijeshi, kwa mujibu wa wizara ya afya.

Waziri mkuu, Youssef Chahed amesema kuwa amempoteza ndugu ambaye alikuwa akitoa huduma ya kibinadamu.

Mbio hizo ziliandaliwa kwenye mji wa pwani wa Nabeul siku ya Jumapili kuchangisha fedha za kujenga zahanati ya watoto ya kutibu ugonjwa wa saratani.

Chaker aliteuliwa kuwa waziri wa afya mwezi uliopita wakati wa mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri.

error: Content is protected !!