August 12, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wazee wakaribia ‘kuula’

Spread the love

MCHAKATO wa utafiti na ukusanyaji maoni ya utungwaji wa sheria ya ustawi wa wazee umefikia hatua ya mwisho na kwamba upatikanaji wa sheria hiyo uko karibuni, anaandika Regina Mkonde

Hayo yamesemwa leo na Fredy Kandonga Afisa Sheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania(LRCT) wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Tunajua Tanzania haina sheria ya ustawi wa wazee inayolinda na kutoa haki za wazee bali ina sera tu ambayo haiwezi ikatetea haki za wazee kisheria mahakamani,” amesema Kandonga.

Ameongeza kuwa “Tume kwa kulijua hilo, kwa mwaka huu wa fedha uliopo tumefanya utafiti pamoja na kukusanya maoni ya wadau mbalimbali juu ya mapendekezo ya utungwaji wa sheria za wazee.”

Kandonga amesema utafiti na ukusanywaji wa maoni umefikia ukingoni na kwamba kilichobaki ni kupelekea maombi kwa waziri mwenye dhamana ya katiba na sheria ili kuufanya mswada hatimaye kupelekwa bungeni na kujadiliwa na wabunge ili uwe sheria.

Amesema sera iliyopo sasa haimsaidii mzee kudai haki zake kisheria na kwamba itakapopatikana sheria itasaidia kuibana jamii kutekeleza majukumu yake ipasavyo katika utekelezaji wa haki za wazee.

Jukumu la LRCT ni kuzipitia sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba kama kutabainika sehemu au vifungu vya sheria vyenye mapungufu na au haziendi na wakati jukumu lao ni kuzirekebisha pamoja na kutoa taarifa zitakazowezesha utungwaji wa sheria mpya.

Aidha, amesema kwa mwaka wa fedha ujao 2017 LRCT imepanga kushughulikia sheria za walaji,mtandao wa kibiashara, sheria za walemavu, kifo, viboko na vifungo vya muda mrefu na kwamba imeshatekeleza jukumu lake la kupeleka taarifa serikalini ili zifanyiwe marekebisho.

Hemed Lusungu ambaye pia ni Afisa Sheria wa LRCT amesema zipo baadhi ya sheria ambazo zimetolewa mapendekezo juu ya ubadilishwaji wake lakini mapendekezo hayo hayajafanyiwa kazi kutokana na kukinzana na mazingira ya makundi mbalimbali.

“Zipo baadhi ya sheria zilizotolewa mapendekezo ya urekebishwaji wake hasa sheria ya ndoa ambayo wadau walijadili kuwa umri sahihi wa binti wa kuolewa ni 21 lakini umri huo huenda ukapngwa kutokana na desturi za baadhi ya makundi ya dini au kabila,” amesema Lusungu.

error: Content is protected !!