Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wazee wa mahakama kuongezewa posho
Habari Mchanganyiko

Wazee wa mahakama kuongezewa posho

Nyundo ya Hakimu
Spread the love

SERIKALI inaangalia uwezekano wa kuongeza posho ya wazee wa mabaraza ya Mahakama kutokana na kiwango cha Sh. 5,000 kinacholipwa hivi sasa kwa wazee hao kuwa kidogo lakini pia kupunguza vitendo vya rushwa, anaandika Dany Tibason.

Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Paramagamba Kabudi alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mbagala, Ali Mangungu (CCM).

Katika swali lake Mangungu alitaka kujua kama setikali haioni kuwa inachochea vitendo vya rushwa kwa kutoa kiasi hicho  kidogo cha posho kwa wazee hao .

Awali katika swali la msingi mbunge huyo alitaka kujua kama serikali haioni ni wakati muafaka sasa kwa serikali kuwaongezea posho wazee hususan katika Mahakama Kuu ya Dar es Salaam ambao wamekuwa wakisikika kesi nyingi zikiwemo za mauaji.

Akijibu swali hilo Kabudi amesema serikali itawaongezea posho wazee wa mahakama kwa kadri bajeti itakavyokuwa inapatikana.

Aidha amesema serikali inatambua mchango mkubwa wa wazee wa baraza katika mahakama nchini na umuhimu wa kutoa posho kama motisha na kwamba kutokana na umuhimu huo serikali ingetamani posho za wazee hao ziongezeke ili kuendana na hali ya uchumi.

Amesema kwa bahati mbaya posho hizo hutokana na bajeti ya matumizi mengineyo ambazo hutengwa na serikali kwa kila fungu.

Hata hivyo Prof. Kabudi amesema kwa mwaka wa fedha 2016/17, mahakama ya Tanzania ilitengewe kiasi cha Sh. 1.27 bilioni na mwaka 2017/18, mahakama imetenga Sh. 1.85 bilioni kwa ajili malipo ya posho ya wazee wa baraza. 

Amesema serikali itaendelea kutenga au kuongeza posho kwa malipo mbalimbali zikiwemo posho kwa ajili ya wazee wa baraza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!