Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari Wazee Hai wamwangukia Rais Samia, waomba Mbowe aachiwe huru
HabariSiasa

Wazee Hai wamwangukia Rais Samia, waomba Mbowe aachiwe huru

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

WAZEE wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, wameiomba Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, imuache huru Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, aliyeko mahabusu kwenye Gereza la Ukonga, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka ya ugaidi …(endelea).

Mbowe ni mzaliwa Hai ambaye ameongoza jimbo hilo kwa nyakati tofauti kwa miaka 15.

Ombi hilo limetolewa na wazee hao jana Jumane, tarehe 3 Agosti 2021, siku 14 tangu Mbowe asote rumande, baada ya kukamatwa na Jeshi la Polisi, usiku wa manane kuamkia tarehe 21 Julai 2021, akiwa hotelini jijini Mwanza.

Salitiael Swai, amemuomba Rais Samia aagize vyombo vya dola vimuache huru Mbowe, akidai kwamba sio gaidi.

“Tunakuomba wewe kiongozi wa nchi usimame katika ukweli, maana uliapa kwamba utashirikiana na watu wote, hutabagua. Mama tunakusihi usibadilishe maneno yako na kama kuna ushauri unatolewa tofauti usikubali, haya mambo yatatuingiza sehemu sio nzuri,” alisema Swai na kuongeza:

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

“Tunaomba shtaka la Mbowe la ugaidi liondolewe mahakamani, mtoto wetu atoke gerezani awe huru tushirikiane nae. Sisi tunamjua ametuongoza Hai kwa muda mrefu, hakuwahi kuwa gaidi, amekuwa mtulivu na mwaminifu siku zote.”

Naye Aishi Mbowe, alimuomba Rais Samia amuache huru Mbowe, kwa kuwa familia yake haina historia ya makosa ya ugaidi, bali ina historia kubwa katika ukombozi wa Tanganyika kutoka kwa wakoloni.

“Familia ya Freeman akiwemo baba yake (Aikael Mbowe), alifanya kazi kubwa ya kupatikana uhuru wa Tanganyika na aliona manyanyaso waliyopata Watanganyika kabla ya kupata uhuru. Ni mtoto aliyefuata nyayo za baba yake kutafuta haki, napata uchungu mwingi kusikia anatuhumiwa kwa ugaidi,” alisema Aishi.

Baada ya kukamatwa jijini Mwanza, Mbowe alisafirishwa kuelekea Jeshi la Polisi la Kanda ya Dar es Salaam, alikohojiwa dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

Tarehe 26 Julai 2021, Mbowe alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka ya ugaidi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba.

Katika mashtaka hayo, Mbowe anadaiwa kula njama na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili shughuli za ugaidi. Inadaiwa alitenda makosa hayo kati ya Mei na Agosti 2020, kwenye Hoteli ya Aishi, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kesi ya Mbowe inatarajiwa kusikilizwa tena mahakamani hapo, kesho Alhamisi, tarehe 5 Agosti 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!