Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari Wazee Dar wamwomba Rais Samia kudumisha utawala bora
HabariHabari Mchanganyiko

Wazee Dar wamwomba Rais Samia kudumisha utawala bora

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

BARAZA la Wazee la Mkoa wa Dar es Salaam, limemuomba Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, aongeze juhudi katika uimarishwaji misingi ya utawala bora. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es salaam..(endelea).

Wito huo umetolewa leo Ijumaa, tarehe 7 Mei 2021 na Salum Matimbwa, Mwenyekiti Baraza la Wazee Mkoa wa Dar es Salaam, katika Mkutano wa Rais Samia na Wazee wa mkoa huo, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City.

“Kuhusu utawala bora, tunakupongeza kwa jinsi ambavyo wewe na serikali yako mnavyosimamia na kutekeleza masulaa mbalimbali ya utawala bora katika nchi yetu, ombi letu tunaomba juhudi hizi ziendelee katika kushughulikia kero za wananchi pamoja na malalamiko yao,” amesema Mzee Matimbwa.

Salum Matimbwa, Mwenyekiti wa Wazee Mkoa wa Dar es Salaam

Wakati huo huo, Mzee Matimbwa ameiomba Serikali ya Rais Samia, iwashirikishe wananchi katika masuala mbalimbali ikiwemo kwenye utafutaji suluhu za changamoto zao.

“Sambamba na hilo, tunaomba vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi kwa kufuata sheria, kanuni na miongozi na pale inapobidi wananchi washirikishwe ipasavyo kuondoa matatizo madogo madogo. Hili kama mnavyo lisimamia vizuri likiendelezwa ustawi wa utawala bora na usalama utaendelea katika nchi yetu,” amesema Mzee Matimbwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!