Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wazee CUF wamlilia Rais Samia madai Katiba mpya
Habari za Siasa

Wazee CUF wamlilia Rais Samia madai Katiba mpya

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

JUMUIYA ya Wazee wa Chama cha Wananchi (CUF) imemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kufufua mchakato wa Katiba mpya pamoja na kuruhusu mikutano ya hadhara ili kurejesha haki kwa vyama vya siasa nchini kutekeleza majukumu yao kikamilifu. Anaripoti Noela Shila – TUDARCo … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 23 Septemba, 2021 na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Mohammed Chunga wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu madai mbalimbali ya chama hicho.

Pia mwenyekiti huyo ameungana na vyama vingine vya siasa kumuomba Rais Samia afufue mchakato wa katiba mpya ili ipatikane Tume Huru ya Uchaguzi nchini.

Amesema kitendo cha kuzuia mikutano ya hadhara ni ukiukwaji wa katiba ya nchi ambayo viongozi wameapa kuilinda.

“Maandamano ni haki ya vyama vya siasa kwa mujibu wa katiba ya nchi ndio maana tunasisitiza viongozi waheshimu katiba.

“Tunaamini mikutano ya hadhara ikirejeshwa, mvutano kati ya polisi na vyama vya siasa ambao umejitokeza katika kipindi cha miaka mitano iliypota hautoendelea,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!