May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wazee CUF wamkingia kifua Profesa Lipumba

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mohamed Chunga

Spread the love

 

JUMUIYA ya Wazee wa chama cha upinzani cha wananchi nchini Tanzania (CUF), kimeonya wale wote wanaoendesha vuguvugu la kumng’oa kwenye nafasi hiyo, Profesa Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho kuacha mara moja. Anaripoti Victoria Mwakisimba TUDARCo … (endelea).

Wazee hao wameibuka kumtetea Profesa Lipumba baada ya kuwapo na mikakati ya kumtaka kujiuzulu wakipinga kile anachokifanya mwenyekiti huyo cha kutengua baadhi ya waliokuwa wakurugenzi mbalimbali wa chama hicho na kuteua wapya.

Leo Alhamisi, tarehe 23 Septemba 2021, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mohamed Chunga amezungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya CUF, Buguruni jijini Dar es Salaam akisema, hatokubali kuona mipango hiyo ikitekelezwa.

Chunga amesema, katiba ya chama ya mwaka 2019 inampa mamlaka mwenyekiti kuteua na kutengua kiongozi hasa pale anapokwenda kinyume na maadili, kukihujumu chama, kushindwa kuwajibika katika nafasi aliyopewa na kwenda kinyume na katiba ya chama.

Amesema kumezuka maneno ya kumtukana mwenyekiti wao ambayo yanaenezwa na baadhi ya wanachama na viongozi wachache huku wakitaka mwenyekiti wao kuachia ngazi hiyo.

Chunga amesema kwa takribani miaka minne chama kimekuwa kwenye mgogoro ambao ulitengenezwa kwa makusudi wakidai Profesa Lipumba sio mwenyekiti wa chama hicho kwa kuwa alijiuzulu mwenyewe.

error: Content is protected !!