Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Wazee Chato wamtwisha mzigo Rais Samia
Habari za Siasa

Wazee Chato wamtwisha mzigo Rais Samia

Mzee Samwel Bigambo,
Spread the love

 

WAZEE wa Wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita, wamemwomba Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kutekeleza ahadi waliyoahidiwa na Dk. John Pombe Magufuli ya kuifanya Chato kuwa mkoa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Chato … (endelea).

Wamesema, enzi za uhai wake akiwa Rais wa Tanzania, Dk. Magufuli kwenye maongezi yao, aliwaeleza anakusudia kuifanya Chato mkuwa mkoa.

Hilo limesemwa na Mzee Samwel Bigambo, wakati akitoa salamu za wazee wa Chato, leo Ijumaa tarehe 26 Machi 2021, kwenye Uwanja wa Magufuli kulikofanyika misa takatifu ya kumwombea Dk. Magufuli.

Kisha mwili wa Dk. Magufuli ambaye ni mzaliwa wa Chato, alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam na mwili wake, utazikwa leo nyumbani kwao Chato.

“Sisi wazee wa Chato, tumefarijika sana kumpa heshima kubwa jemedali wetu baada ya kuwa amekufa na kumzungusha karibu Tanzania nzima na kumfikisha kwetu Chato.”

“Tunahuzuni sana kwa kuondokewa na kijana wetu na mpenzi wetu lakini kimepangwa na Mungu, tukizidi kulia sana tutakuwa tunakufuru kwa hiyo tunashukuru kwa kila jambo,” amesema Mzee Bigambo

Mzee huyo amesema, mmetuenzi kwa kutuletea huu ugeni, “mmemuenzi Mjane wetu, Janeth Magufuli na mama haya ni mapenzi ya Mungu na kufanya hivyo ni mapenzi yake.”

Mara baada ya kifo hicho, aliyekuwa makamu wake wa Rais, Samia Suluhu Hassan, aliapisha tarehe 19 Machi 2021 kuwa Rais wa Tanzania na leo Ijumaa yupo Chato kushiriki maziko ya Dk. Magufuli.

“Tunaomba serikali iliyobaki, iwe karibu sana na Mjane Janeth kwa sababu ana kipindi kigumu kwa sasa,” amesema.

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania

Mzee Bigambo amesema, wao wazee wa Chato “tulishindwa hata kumwelea kazi zake alizozifanya, tuliitwa ni nchi masikini lakini kwa muda mfupi akawa anafanya miradi mingi, sijui alifungua wapi zikawa zinatoka hela, ameondoka kimwili lakini fikra hazitatoka.”

“Wazee wa Chato tunamatumaini kwamba, hakuwa peke yake bali alikuwa na mwenzake, Samia Suluhu Hassan na tuna imani, miradi yooooote ataitekeleza na kuongeza mingine. Kipimo cha uongozi wowote ni kipimo cha uongozi uliopita kwa hiyo mama (Samia), tutakupima kwa uongozi uliopita,” amesema

Akigusia suala la Chato kuwa Mkoa, Mzee Bigambo amesema “Chato siku moja aliwahi kutuambia hii Chato tunataka tuifanye iwe mkoa, sasa je, hiyo ahadi ife? Haiwezi kufa kwa sababu wewe (Rais Samia) ulikuwepo.”

Huku waombolezaji wakifurahia hilo, Mzee Bigambo amesema ” tuna matumaini makubwa na kwa uzoefu wangu katika maisha yangu na mara nyingi huwa tunasema kuliko mtoto kufa, tunasema afe mama.”

“Kwa sababu hata kama mtakataa, miji inayoachiwa wananume huwa inaharibika lakini miji inayoachiwa wanawake huwa inaendelea na mimi naamini mama yetu atatufanyia mazuri zaidi,” amesema Mzee Bigambo huku Rais Samia akionekana kutabasamu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!