Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Wazee Chadema wajitosa sakata la Mbowe, wajitosa madai katiba mpya
Habari

Wazee Chadema wajitosa sakata la Mbowe, wajitosa madai katiba mpya

Spread the love

BARAZA la Wazee la chama kikuu nchini Tanzania cha Chadema, limeiomba Serikali imfutie mashtaka ya kula njama za kufanya ugaidi, yanayomkabili kiongozi wa chama hicho, Freeman Mbowe na wenzake watatu, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Anaripoti Victoria Mwakisimba, TUDARCo … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumanne, tarehe 17 Agosti 2021 na Katibu Mkuu wa baraza hilo, Roderick Lutembeka, akizungumza na wanahabari kao makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi na kula njama za kufanya ugaidi Na. 63/ 2021, ni Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohammed Abdillah Lingwenya.

“Tunaendelea kusisitiza Mbowe sio gaidi na hivyo tunamtaka Rais Samia na Serikali yake waachane na haya mashtaka, kwani yanazidi kuligawa Taifa na kulibomoa,” amesema Lutembeka.

Lutembeka amesema, mustakabali wa Tanzania utapatikana kwa njia ya mazungumzo na sio kushindana “ndani ya Chadema sisi wazee tunaamini, mustakabali wa Taifa hili hautapatikana kwa mashindano.”

Aidha, Lutembeka amemuomba Rais Samia akutane na wazee wa baraza hilo, ili wazungumzie mustakabali wa Tanzania.

“Tungependa kumkumbusha rais barua aliyoandikiwa na chama na tulifarijika alipoijibu hiyo barua ya kukutana na wazee, kwa ajili ya mazungumzo ili kuleta utengamano kitaifa.”

“Lakini bahati mbaya sana yaliyotokea yametokea. Tunaamini busara na hekima inaweza kufanyaika ili kukaa na kuleta msutakabali wa Taifa hili,” amesema Lutembeka.

Mbali na wito huo kwa Rais Samia, Lutembeka ametoa maagizo kwa wazee wa baraza hilo nchi nzima, akiwataka wabebe jukumu la kudai katiba mpya.

“Tunachukua nafasi hii kuwaelekeza wazee wa baraza nchini kote, sisi tuongoze njia kuhakikisha kuwa tunaipata katiba mpya kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho,” amesema Lutembeka.

Lutembeka ameongeza “tusikubali kurudishwa nyuma na kikundi kichache ambao wanang’ang’ania katiba iliyopo, sababu inawasaidia kuingia madarakani pasipo kufuata demokrasia.”

Lutembeka amesema, upatikanaji katiba mpya utaondoa changamoto zinazoikabili Tanzania.

“Wananchi walitoa maoni yao kwa miaka miwili wakionesha wanataka katiba ya aina gani, kwani iliyopo imepitwa na wakati na imekuwa na mapengo mengi. Hili halina ubishi,” amesema Lutembeka.

Ajenda ya kudai katiba mpya, ilikuwa inashikiliwa na Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), ambalo liliandaa makongamano kadhaa ya kushinikiza ufufuaji mchakato wa upatikanaji katiba hiyo, uliyokwama Aprili 2015.

Harakati za Bavicha kudai katiba mpya, zilikwama baada ya Mbowe na wenzake kukamatwa usiku wa kuamkia tarehe 21 Julai 2021, wakiwa hotelini jijini Mwanza, wakijianda kushiriki kongamano la kudai katiba mpya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariMichezo

Benki ya NBC yazindua kombe jipya la Ligi Kuu Tanzania Bara

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa Ligi ya NBC , Benki ya Taifa...

AfyaHabariHabari

Ugonjwa wa ajabu wadaiwa kuua watano Kagera, Serikali yatoa tahadhari

Spread the loveJUMLA ya watu watano wanaidaiwa kufariki dunia  katika vijiji vya...

ElimuHabari

Shule ya Hazina yaanza kutoa elimu bure

Spread the loveKATIKA jitihada za kuunga mkono serikali ya awamu ya sita...

AfrikaHabari

Majenerali 35 kustaafu kutoka jeshi la Uganda

Spread the loveTAKRIBANI majenerali 35 wanatarajia kustaafu kutoka jeshi la Uganda (UPDF)...

error: Content is protected !!