Tuesday , 18 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wazee ACT-Wazalendo watoa neno maandalizi uchaguzi 2019
Habari za Siasa

Wazee ACT-Wazalendo watoa neno maandalizi uchaguzi 2019

Bendera ya ACT-Wazalendo
Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kupitia ngome yake ya wazee, kimetoa msimamo kuhusu ushiriki wake katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 6 Julai 2019, Yeremia Maganja, Mwenyekiti wa Ngome ya Wazee ACT-Wazalendo, amesema chama hicho kitashirikiana na vyama vingine vya siasa, ili kuhakikisha vyama vya upinzani vinanyakua ushindi kwenye uchaguzi huo.

Maganja ameeleza mikakati ya ushindi katika uchaguzi huo, ikiwemo kuhakikisha mazingira ya uchaguzi huru na wa haki yanakuwepo, ikiwemo upatikanaji wa Tume Huru ya Uchaguzi.

Amesema kupatikana kwa Tume Huru ya Uchaguzi kutasaidia kuondoa changamoto ya ukiukwaji wa misingi ya katiba na sheria, katika mchakato wa uchaguzi.

Wajumbe wa Ngome ya Wazee ya ACT-Wazalendo kutoka mikoa mbalimbali wamekutana leo jijini Dar es Salaam,  kwa ajili ya kushiriki katika kikao cha kikosi kazi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mazingira magumu ya JPM yamechangia ‘Comedy Journalism’

Spread the loveMwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia hali ya uchumi wa vyombo...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Nimeacha ubabe

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia atoa ujumbe mzito Sikukuu Eid Al Adha

Spread the loveKATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha, Rais wa Tanzania,...

BiasharaHabari za Siasa

Dk. Biteko aipongeza NMB kwa kuanzisha utoaji wa bima ya mifugo

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!