Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wazee ACT-Wazalendo: Tusilaumiane
Habari za SiasaTangulizi

Wazee ACT-Wazalendo: Tusilaumiane

Spread the love

SIKU moja baada ya Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazakendo kusema ‘tusilaumiane’, kauli hiyo imerejewa na wazee wa chama hicho. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Wazee hao wametoa kauli hiyo kwa madai ya kuchoshwa na hila, ghiliba na mikakati inayofanywa na wasimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Leo tarehe 10 Novemba 2019,
Hemedi Tau, katibu wa wazee hao amesema, watahamasisha wafuasi na wananchi kutotii viongozi watakaotokana na uchaguzi huo.

Tau amemtaka Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jaffo kuondoa majina ya wagombea waliojitoa kwenye uchaguzi huo.

“Tanzania hakuna mfumo wa mgombea binafsi, mgombea ambaye chama chake kimekoma kumdhamini au yeye mwenyewe amejiondoa kwa barua, hawezi kuwa mgombea halali kwenye uchaguzi.

“Kwa vile CCM kinahofia uchaguzi, ni vema Waziri Jaffo angetangaza kuwa kimepita asilimia mia,” amesema Tao.

Amesema, hivi karibuni chama hicho kitatangaza hatua watakazo chukua.

“…Huko mbele yatakayotokea tusije kulaumiana, kuna hatua zitakazochukuliwa…” amesema.

Twaha Taslima, Mwanasheria Mkongwe na mjumbe wa Ngome hiyo amesema, haijawahi kutokea kitendo cha aina hiyo kipindi chote cha historia ya Tanzania.

“Hiki kitu sio cha kisiasa wala sio cha kisheria, kwasababu haiwezekani na haijawahi kutokea uchaguzi wa namna hii katika nchi yetu,” amesema Taslima.

Amesema, haikuwa kutokea chama cha siasa kikijiondoa kwenye uchaguzi, halafu wenye mamlaka wakalazimisha kuwa bado kipo.

ACT-Wazalendo kimeungana na Chadema kugomea uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba 2019, kwa madai ya kutawaliwa na hila.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!