August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wazazi watakiwa kutonyanyasa watoto

Spread the love

WAZAZI nchini wametakiwa kuacha tabia ya kunyanyasa watoto bali wawatimizie haki na mahitaji yao kwa mujibu wa sheria zilizopo, anaandika Christina Haule.

Ally Mlango, Ofisa Elimu wa Kata ya Mtibwa amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mdahalo wa wazi wa kuwaelimisha wanafunzi juu ya masuala ya kupinga ukatili wa kijinsia kwenye mradi wa kupinga ukatili wa kijinsia (GEWE II).

Mridi huo umeandaliwa na Chama cha waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa ufadhili wa Shirika la Msaada la Denmark (DANIDA) na ambapo umefanyika Morogoro.

Mlango ambaye pia ni Kaimu Ofisa Mtendaji wa kata hiyo amesema, vitendo viovu vinavyosababisha ukatili wa kijinsia hufanywa kwa wanafunzi pindi wawapo majumbani mwao au kwa jamii zinazowazunguka.

“Wapo baadhi ya wazazi huwanyanyasa watoto pengine kutokana na ugumu wa maisha au la, sababu utakuwa mzazi anamuadhibu sana mtoto aliyekula mboga yote au chakula chote bila kujali kuwa atamuumiza kwa kiasi gani,” amesema.

Monica Kibena, Mwalimu wa Shule ya Msingi Madizini B amewashauri wanafunzi wa shule kutoogopa kutoa taarifa pindi wanapoona mwenzao kafanyiwa ukatili wa aina yoyote.

error: Content is protected !!