September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wazazi watakiwa kushirikiana na walimu kuwajenga watoto

Wanafunzi wakiwa darasani

Spread the love

WAZAZI pamoja na walezi wametakiwa kujenga utamaduni wa kushirikiana na walimu ili kuweza kuwajenga watoto katika malezi bora. Anaripoti Danson Kaijage, Moshi … (endelea).

Hayo yameelezwa na Meneja msaididi ya shule ya msingi ya Goodshepherd, iliyopo Himo mjini Moshi, Erica Chilewa alipokuwa akizungumza na MwanaHALISI Online juu ya ushirikiano kati ya wazazi na walimu.

Erica amesema kuwa ili kupata taifa lenye watu makini ni lazima mtoto aanze kujengewa misingi bora tangu akiwa Mtoto.

Kiongozi huyo wa shule ya msingi ya binasfi,amesema kuwa wazazi wanawajibu wa kushirikiana na walimu katika kukuza maendeleo ya mtoto pamoja na kumjengea mazingira bora ya mimakuzi.

“Wazazi na walezi wanatakiwa kuwa karibu sana walimu na kwa kufanya hivyo kunamfanya mwanafunzi kutambua kuwa hiwapo atafanya jambo baya lenye viashiria vya utovu wa nidhamu ni wazi kuwa atanulikana na atapewa adhabu au onyo toka pande zote.

“Pia ikumbukwe malezi bora kwanza yanaanzia katika familia husika na wazazi wengi wamekuwa chanzo cha kushusha maadili ya watoto wao kwa kukosa nafasi ya kukaa na watoto kuwasikiliza au kujua mwenendo wa masomo yao.

“Wakati mwingine mafarakano na lugha ambazo hazina staha kwa wanafamilia mbele ya watoto wao zinawafanya watoto kuwa wakosefu wa adabu kwani wanajifunza mambo mabaya kutoka kwa walezi wao au wazazi wao,” amesema Erica.

Katika hatua nyingine amewahimiza wazazi kuhakikisha wanawapatia watoto wao elimu iliyo bora na si bora elimu kwa faida ya watoto wenyewe na faida kwa taifa.

Shule ya msingi ya Goodshepherd inatarajia kufanya mahafari yake ya kwanza ya darasa la saba leo huku mgeni rasm anatarajiwa kuwa Afisa Tawala wa halmashauri ya Moshi akimwakirisa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde.

error: Content is protected !!