March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wazazi, walezi wapewa neno

Neema Rusibamaiya, Mkurugenzi wa Huduma ya Chanjo wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia Wazee na Watoto

Spread the love

WAZAZI na walezi kuwatunza na kiwalea watoto wa chini ya miaka mitano ikiwamo kuwapatia lishe bora, elimu na kuwalinda dhidi ya unyanyasaji, anaandika Angela Willium.

Kauli hiyo imetolewa leo na Taasisi ya Maendeleo ya Binadamu Chuo Kikuu cha Aga Khani na kusisitiza kuwa hatua hiyo itawasaidia watoto hao kukua.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma ya Chanjo katika Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Neema Rusibamaiya amewataka wazazi wanatakiwa kuwapatiwa watoto lishe bora, kukaa nao pamoja, kucheza nao na kuwasemesha hata kama hawajaanza kuongea kwa kuwa hatua hiyo inasaidia kuwakuza kiakili.

‘’Familia inatakiwa kuwalinda watoto dhidi ya watu wanaowanyanyasa kwa kuwa wanasababisha maendeleo yao kurudi nyuma hivyo kama kuna unyanyasaji mzazi asikae kimya.’’

Aidha, mwakirishi wa taasisi ya Aga Khan, Leonard Chumo amesema wamewekeza katika masuala ya elimu, afya na lishe bora lengo likiwa ni kuangalia haki za watoto chini ya miaka 5.

Chumo amesema wadau kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Uganda , Kenya na serikali wamekutana leo katika kujadili namna ya kuwasaidia watoto ili waweze kukua vizuri.

error: Content is protected !!