August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wazazi CCM walilia posho

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi la Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, kimetakiwa kuona umuhimu wa kuithamini Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho sambamba na kuwalipa posho makatibu wake kwani wamekuwa wakitekeleza majukumu yao bila kupewa fedha yoyote, anaandika Christina Haule.

Mwajuma Salim, Katibu wa jumuiya hiyo wilaya ya Morogoro Mjini amesema hayo wakati akisoma taarifa fupi ya kazi na uhai wa Jumuiya ya Wazazi katika wilaya hiyo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Septemba mwaka 2016.

Mwajuma amesoma taarifa hiyo mbele ya Josephat Chacha, katibu wa jumuiya hiyo Mkoa wa Morogoro ambapo amedai kuwa makatibu hao wanapaswa kupata posho ili kuongeza morai ya kazi kama makatibu wa chama wanavyopewa.

“Tunaomba suala hili la posho lizingatiwe kwani tunafanya kazi kubwa ya kukijenga chama katika ngazi mbalimbali bila kupewa chochote na pia tunakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo baadhi ya viongozi wa serikali kukidharau chama na jumuiya zake jambo linalovunja nguvu ya kufanya kazi,” amesema.

Awali Chacha ambaye ni katibu wa jumuiya hiyo mkoa aliwasihi viongozi CCM kujenga tabia ya kufanya vikao mara kwa mara ili kuhakiki uhai wa chama.

“Vikao vina uwezo mkubwa wa kuimarisha chama kufuatia wanachama wengi kutambulika na kuona umuhimu wa kulipa ada zao kwa wakati jambo litakalosaidia kuongeza mapato na kuboresha maendeleo ya jumuiya ya Wazazi,” amesema Chacha.

error: Content is protected !!