March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wazazi Azania sekondari watupiwa neno

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Azania

Spread the love

WAZAZI wa shule ya sekondari Azania wanaombwa kuchangia fedha kwa ajili ya kununua viti vya kukalia wanafunzi wanapokuwa darasani, anaandika Angel Willium.

Akizungumza na wazazi hao Mkuu wa shule hiyo, Erasto Guimili katika mahafalii ya kidato cha nne leo jijini Dar es salaam amesema wazazi wanatakiwa kutoa kipaumbele katika kuchangia viti vya kwa ajili ya watoto wao.

Amewataka wazazi ho kuhudhuria mikutano ya shule ili kujua maendeleo ya watoto wao.

Aidha, Ofisa elimu wa kata ya Upanga Mangaribi, Emaculath Ngule amewaomba wadau mbalimbali kujitotekeza kuchangia shule hiyo kwani vilivypo vimechakaa.

Leo shule hiyo leo imeadhimisha mahafali ya 81 tangu kuazishwa kwake na kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 1436.

error: Content is protected !!