December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wazambia wamuaga Sata

Mazishi ya Rais wa Zambia Michael Sata

Spread the love

MAELFU kwa maelfu ya wananchi wa Zambia, wameshiriki katika kumuaga aliyekuwa kiongozi wao mkuu, Rais Michael Chilufya Sata.

Rais Satta aliyefariki dunia 28 Oktoba, mjini London, nchini Uingereza, ambako alikwendwa kwa matibabu.

Mazishi ya Rais Sata yamefanyika Jumanne, 11 Novemba 2014, katika makaburi rasmi yaliyotengwa kuzikwa viongozi wakuu wa taifa, linaloitwa Embassy Park, mjini Lusaka.

Mwili wa rais Sata uliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, Lusaka, Jumamosi, tarehe 1 Novemba 2014, kutokea nchini Uingereza.

Mara baada ya mwili huo kuwasili nchini humo, ulipelekwa katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mulungushi, ambako wananchi wa Zambia na wageni wengine mashuhuri, walipata fursa ya kumuaga.

Kaimu Rais, Dk. Guy Scott, aliweka shada la maua katika jeneza la rais.

Kwa mujibu wa taarifa ya serikali, misa ya kumuaga rais Sata, itafanyika Jumannne, tarehe 11 Novemba 2014, katika viwanja vya mashujaa, mjini Lusaka. Baadaye mwili wake, utapelekwa Embassy Park kuhifadhiwa kwa safari ya milele

Rais wa kwanza wa Zambia, kati ya mwaka 1964 – 1991, Dk. Kenneth Kaunda, alionekana mwenye huzuni kubwa, wakati alipotoa heshima zake za mwisho kwa rais Sata. Alishindwa kujizuia kumwaga chozi hadharani.

Dk. Kaunda, alikuwa miongoni mwa wannachi waliojitokeza kumuaga rais Sata.

Kiongozi huyo wa kwanza wa Zambia, alishindwa kujizuia kumwaga machozi hadharani, kumlilia rais wake.

.

Baada ya uhuru wa Zambia kutoka kwa Waingereza (1964), Sata alijiunga na chama tawala cha Muungano wa kitaifa wa Uhuru – United National Independence Party (UNIP). Katika miaka ya 80, Sata alikuwa gavana wa Lusaka.

Baadaye akajitenga na UNIP na kujiunga na vuguvugu la demokrasia ya vyama vingi lililojulikana kwa jina la Movement for Multi-Party Democracy (MMD).

Baada ya MMD kushinda serikali, Sata alifanywa kuwa waziri katika wizara kadhaa, ikiwamo Serikali za Mitaa, Kazi, Afya na Waziri asiyekuwa na wizara maalumu.

Mwaka 2001 alijiondoa katika chama hicho. Akaunda chama chake cha Patriotic Front. Mwaka 2011 kupitia chama hicho, Sata alipata ushindi wa karibu asilimia 42 ya kura.

Kwa mujibu wa Katiba ya Zambia, Kaimu Rais, Dk. Scott, haruhusiwi kugombea urais katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwaka kesho. Kisa: Wazazi wake, ni raia kutoka Uskochi, ingawa mwenyewe ni raia wa Zambia, tena wa kuzaliwa.

Hii ni baada ya aliyekuwa Rais wa Pili wa Zambia, Fredrick Chiluba, kufanyia Katiba ya nchi hiyo, mabadiliko yaliyolenga kumzuia Rais Kaunda kurejea katika mbio za urais.

Chiluba aliingia Ikulu mwaka 1991, baada ya kumshinda Dk. Kaunda. Chiluba alihofu kuwa gwiji hilo la siasa nchini mwake, ligejitosa katika kinyang’anyiro hicho tena.

Akaamuru kuwekwa kwenye katiba, kifungu kinachosema, “Ili uwe rais ni lazima wazazi wako wote wawe wazaliwa wa Zambia.” Baba wa Kaunda, alikuwa raia kutoka Malawi.

Baada ya kushinda urais, Chilumba alimsweka gerezani rais Kaunda; jambo ambalo lililaaniwa na nchi zote marafiki. Lakini mungu si Athumani. Naye alifikishwa mahakamani na Mwanawasa, mtu ambaye alimteuwa kuwa mrithi wake na kushiriki kumpigia kampeni kwa tuhuma za kuhusika katika rushwa.

Sata aliyezaliwa mwaka 1937 katika eneo la Mpika lililopo Kaskazini mwa nchi hiyo, anakuwa rais wa pili wa nchi kufariki dunia akiwa madarakani. Mwingine aliyefariki dunia akiwa madarakani, ni Levy Mwanawasa. Alikuwa Rais wa tatu wa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa madini ya dhahabu barani Afrika, kufariki akiwa mamlakani. Alifariki 3 Julai 2008.

Mwanawasa alifariki katika kipindi cha pili cha uongozi wake kutokana na ugonjwa wa ghafla wa mapigo ya moyo.

Baada ya kifo cha Mwanawasa, Rupiah Banda alichukua madaraka ili kumalizia muda wake wa uongozi.

Lakini baada ya miaka mitatu, rais Banda wa Zambia alipoteza nafasi yake iliyochukuliwa na aliyekuwa kiongozi mkongwe wa upinzani nchini humo – Michael Sata.

error: Content is protected !!