Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wazalishaji mbogamboga, matunda kunufaika na soko Ulaya
Habari Mchanganyiko

Wazalishaji mbogamboga, matunda kunufaika na soko Ulaya

Spread the love

 

TANZANIA imejumuishwa kwenye orodha ya nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) zitakazonufaika na utekelezwaji wa Programu mpya ya Fit for Market Plus inayolenga kuwajengea uwezo wajasiriamali na wale wote wanaojihusisha na mnyororo mzima wa uongezaji thamani katika mazao ya kilimo, hususan mbogamboga na matunda. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Program hiyo itawezesha wakulima kuzalisha mazao na bidhaa za kilimo zinazokidhi viwango na mahitaji ya soko, hususan la Umoja wa Ulaya.

Programu hiyo inayotekelezwa na taasisi ya COLEACP kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya inazingatia Mkakati wa Umoja huo ujulikanao kama Farm to Fork Strategy unaolenga kudhibiti ubora wa bidhaa za mazao ya kilimo zinazoingia kwenye soko kuanzia shambani mpaka zinapomfikia mlaji wa mwisho.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiana wa Kimataifa inatoa wito kwa wadau wote wanaojihusisha na mnyororo wa uongezaji thamani katika mazao ya kilimo cha mbogamboga na matunda kuchangamkia fursa kwa kujitokeza kwa wingi kuwasilisha maombi yao ya kunufaika na utekelezwaji wa programu hiyo.

Wadau hao ni pamoja na kampuni na vikundi vinavyojihusisha na uzalishaji na uuzaji wa mazao ya mbogamboga na matunda; taasisi zinazojihusisha na utoaji mafunzo na ushauri wa kitaalamu kuhusu kilimo cha mbogamboga na matunda; mamlaka zenye dhamana ya usimamizi wa afya ya mimea; na taasisi za utafiti katika kilimo cha mbogamboga na matunda.

Kwa maelezo zaidi kuhusu namna ya kunufaika na utekelezwaji wa programu hiyo, wadau wanashauriwa kutembelea tovuti ya COLEACP: https://www.coleacp.org/current-programmes/fit-for-market-plus/. Wanaweza pia kuwasiliana moja kwa moja na COLEACP kupitia barua pepe support@coleacp.org.

Kupatikana kwa fursa hiyo ni jitihada za Ubalozi wa Tanzania nchini Ubelgiji katika mikakati yake ya utekelezaji wa diplomasia ya uchumi ambao unawahimiza pia wadau kutembelea tovuti: www.be.tzembassy.go.tz ili kupata taarifa zaidi kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye eneo la uwakilishi la ubalozi huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

error: Content is protected !!