October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wawili Yanga, kuikosa Biashara United leo

Spread the love

 

KLABU ya Soka ya Yanga hii leo itashuka dimbani kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Biashara United kutoka mkoani Mara, kwenye muendelezo wa michuano ya kombe la Shirikisho la Azam. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo wa hatua ya mtoano, utapigwa hii leo kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaa, majira ya saa 1 usiku ambapo Yanga ndio atakuwa mwenyeji.

Yanga wanashuka dimbani kwenye mchezo huo, huku wakiwa na kumbukumbu ya kufika fainali kwenye michuano hiyo kwa msimu uliopita na kupoteza kwa bao 1-0, mbele ya Simba kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Katika mchezo huo, wachezaji wawili wa kikosi cha kwanza wa klabu hiyo, Dikson Job sambamba na Djuma Shabani watakosa mchezo huo kutokana na kukabiliwa na adhabu, kufuatia kufungiwa na kamati ya usimamizi na uwendeshaji wa Ligi (kamati ya Saa 72).

Djuma Shabani yeye alifungiwa michezo mitatu na kupigwa faini ya shilingi 50,000 kufuatia kumpiga kwa kiwiko mchezaji wa Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi kuu ulipigwa kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Huu utakuwa mchezo wa mwisho kwa mlizni huyo wa kulia raia wa Jamhuri ya Congo, kufuatia kukosa michezo miwili iliyopita dhidi ya Mbao na Mbeya City.

Kwa upande wa Dikson Job yeye ndio ataanza kuitumikia adhabu yake kwenye mchezo huo, mara baada ya kufungiwa michezo mitatu na kupigwa faini ya shilingi 50,000 na kamati hiyo.

Yanga na Biashara mara ya mwisho kukutana kwenye michuano hii, ilikuwa msimu uliomalizika kwenye hatua ya nusu fainali, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, mchezo uliopigwa mkoani Mara.

error: Content is protected !!