January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wawili wakamatwa na meno ya Tembo

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekamata watuhumiwa wawili waliokutwa na meno ya Tembo 156. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na wanahabari Kamanda wa Kanda Maalumu ya Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema kuwa meno hayo yenye uzito wa Kilo 211.66, yamekamatwa Mtaa wa Miburani, Temeke jijini Dar es Salaam.

Nyumba iliyokutwa na meno hayo ndimo anamoishi mmoja wa watuhumiwa, Ramadhan Mnekea (55)  ambapo mtuhumiwa wa pili Robert Isack (32) anaishi Mabibo, Dar es Salaam.

Watuhumiwa hao wamekamatwa Desemba 21 walipokuwa kwenye mikakati ya kusafirisha meno hayo maeneo ya Temeke Sudani jijini Dar es Salam baada ya raia wema kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.

Kova amesema kuwa shauri la kesi hiyo litakadhiwa kwa mwanasheria wa serikali baada ya kukamilika kwa upelelezi huo ambapo jeshi hilo linashirikiana na maofisa wa Idara ya Wananyamapori.

Naye Mkuu wa Polisi Wilaya ya Temeke, Andrew Sata amewapongeza raia wema walioshirikiana na jeshi hilo kuwafichua wahalifu licha ya kutoa wito kwa wananchi wengine kufichua wahalifu na kuwataka wananchi wanaoishi karibu na hifadhi mbalimbali nchini kufichua wahalifu kama hao

error: Content is protected !!