Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Wawili mbaroni tuhuma kuua madereva, kupora pikipiki
Habari Mchanganyiko

Wawili mbaroni tuhuma kuua madereva, kupora pikipiki

Kamanda Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Jumanne Murilo
Spread the love

 

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia watu wawili, kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya madereva wawili kisha kupora pikipiki ‘Bodaboda’. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, ACP Jumanne Muliro, amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Iddi Omari Ngakae na Mfaume Donald Kapela.

Kamanda Muliro amedai kuwa, watuhumiwa hao walitekeleza tukio la kwanza tarehe 16 Aprili 2022, ambapo walimkodisha dereva wa bodaboda, marehemu Jumanne Mpenja, kutoka Mbagala Charambe kwenda Kigamboni, ambapo walipofika kwenye visiki walimpiga na kitu kizito kichwani na hatimaye kufariki.

“Katika mahojiana ya kina na mtuhumiwa huyo, Jeshi la Polisi lilibaini kuwa alishiriki katika tukio lingine la kumpiga kwa kitu kizito kichwani kisha kumuua, Mkapa Nuru miaka (20-25) tarehe 27 Agosti 2021, aliyekuwa mkazi wa Mbagala Kiburugwa na kumpora pikipiki namba MC186 CXX aina ya Boxer,” amedai Kamanda Muliro na kuongeza:

“Baada ya kufanya tukio hilo la mauaji, mtuhumiwa aliutupa mwili eneo la Visikini Dege Kigamboni, ambapo katika ukaguzi wa eneo hilo kumepatikana mifupa idhaniwayo ya binadamu ambayo ni fuvu la kichwa, mifupa mwili ya nyonga na kaptula ya jeans, vyote vinavyodhaniwa kuwa ni vya marehemu aliyekuwa anatafutwa muda mrefu.”

Katika hatua nyingine, Kamanda Muliro amesema wanawashikilia watu 10 akiwemo Abdulaziz Abdallah (19), mkazi wa Chanika Tungini, kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kujeruhi watu kwa mapanga, kuvunja nyumba usiku na kuiba katika maeneo mbalimbali ya jiji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

error: Content is protected !!