December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wawili mbaroni kwa kuuza biskuti, pipi zenye bangi

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Gerald Kusaya

Spread the love

 

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imewakamata watu wawili jijini Arusha kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya kuuza biskuti na pipi zilizotengenezwa kwa dawa za kulevya aina ya bangi.

Watuhumiwa hao ni Abdulnasir Haruon Kombo (30) mfanyabiashara wa Kaloleni jijini Arusha na Hassan Ismail (25) mkazi wa Olasiti jijini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kombo amekamatwa akiwa na biskuti 50 zilizotengenezwa kwa kutumia dawa za kulevya aina ya bangi kama moja ya malighafi akiwa anaziua katika eneo la Kaloleni jiji Arusha wakati Ismail ndiye anayesadikiwa kuwa ndiye mtengenezaji wa biskuti hizo zenye dawa za kulevya aina ya bangi.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 15 Novemba, 2022 na Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo, Gerald Kusaya amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kutokana na operesheni iliyofanywa kuanzia Oktoba na mwanzo mwa Novemba mwaka huu.

Amesema watuhumiwa hawa wameshafikishwa mahamani jijini Arusha.

Aidha, amesema matukio ya uwepo wa bidha za vyakula vinavyotengenezwa kwa kutumia bangi yameanza kushamiri nchini.

“Itakumbukwa kuwa mwaka 2020, 2021 Mamlaka ilikamata bangi iliyosindikwa mfano wa jam, keki na asali katika matukio tofauti wakati wa utekelezaji wa operesheni zake.

“Hali hii inaonesha wazi kuwa tatizo hili limeanza kushamiri nchini na hasa ikizingatiwa kuwa wafanyabiashara hawa wenye nia ovu hutumia vyakula vinavyopendwa na watoto mfano wa pili, keki, ice creram na biskuti hivyo kuwapo na uwezekano wa kuwaingiza watoto kwenye matumizi ya dawa za kulevya bila kujua na hatimaye kuwa waraibu,” amesema.

Kutokana na hali hiyo ametoa wito kwa wazazi na walezi kufuatilia kwa ukaribu nyendo za watoto wao.

“Mammlaka inawakumbusha wananchi kuwa kujihusisha kwa namna yoyote ile na dawa za kulevya ni kosa kisheria. Sheria ya kuthibiti na kupambana na dawa za kulevya sura ya 95 inatoa ahdabu kali hadi kifungo cha maisha kwa atakayethibitika kujihusisha na kosa hilo.

“Nitoe wito kwa wananchi kushiriki kwa dhati katika kukabiliana na tatizo la matumizi na biashara ya dawa za kulevya kwa kuwafichua wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo,” amesema.

error: Content is protected !!