August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wawili kizimbani kwa meno ya tembo

Spread the love

WATU wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa kosa la kusafirisha meno ya tembo kiasi cha kilogram 3500 yenye thamani ya zaidi ya  Sh 4.2 bilion, anaandika Faki Sosi.

Watuhumiwa hao ni Kassim Said kwa jina maarufu Bedui (50) Mkazi wa Arusha na Joachim Minde (Kennedy Kimaro) (55) Mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam.

Akisoma mashtaka hayo leo Salim Msemo, Wakili wa Serikali mbele ya Amilius Mchauru, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo amedai kuwa, watu hao wanakabiliwa na mashtaka mawili.

Msemo amedei kuwa, watuhumiwa hao walijihusisha na genge la wahalifu na kudaiwa, kati ya Machi 2013 na Agosti  2015 walijihusisha na genge la uhalifu la kusafirisha nyara za serikali bila kibali cha Ofisi ya Wanyamapori.

Shitaka la pili linalowakabili watuhumiwa hao ni kusafirisha nyara za serikali ambazo ni vipande vya meno ya tembo kilo 3500 venye thamani ya Shilingi 4,202,275,000 walivyokuwa wakivisafirisha kutoka nchini hadi Hong Kong, China na Thailand bila ya kibali kutoka mamlaka husika kitendo ambacho kinyume na sheria.

Upande wa utetezi umedai kuwa, upelelezi haujakamillika. Watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote katika mashitka hayo kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo bila ya kibali cha Mwendesha Mashtaka (DPP). Kesi hiyo itatajwa tena  tarehe 10 Oktoba mwaka huu.

 

error: Content is protected !!