Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Wawili wafariki dunia ajalini Pwani
Habari Mchanganyiko

Wawili wafariki dunia ajalini Pwani

Spread the love

WATU wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa, katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 4 Septemba mwaka huu, iliyohusisha magari mawili ambayo yamegongana uso kwa uso katika barabara ya Dar es Salaam -Morogoro eneo la Mbala, Chalinze Mkoani Pwani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani,(ACP) Wankyo Nyigesa akisema kuwa imetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 9.30 alfajiri.

Akielezea kuhusu tukio hilo, ACP Nyigesa amesema gari namba T.542 DMJ/ 680 DKS aina ya Howo mali ya kampuni ya Gulf Agent ikitoka Dar es salaam kuelekea Chalinze ikiendeshwa na dereva Ramadhani Kibingo ( 38) mkazi wa Mbagala iligongana na gari T.405 DLV/ 904 DMN aina ya Daf mali ya kampuni ya RAS Logistic (T) ltd iliyokuwa ikitokea Morogoro kuelekea Dsm ikiendeshwa na dereva ambaye jina lake bado halijafahamika.

Amesema waliofariki dunia ni dereva huyo wa gari yenye namba T.405 DLV/904 DMN aina ya Daf na tingo wake ambao bado majina yao hayajafahamika.

Wankyo aliwataja majeruhi kuwa ni dereva Ramadhani Kibingo na tingo wake Ibrahim Said, Mzigua (28), mkazi wa Dar es salaam waliokuwa ndani ya gari T.542DMJ/680 DKS.

Miili ya marehemu imepelekwa hospital ya rufaa Tumbi kwa uchunguzi na kuhifadhiwa na majeruhi wamepelekwa kituoa cha afya Chalinze kwa ajili ya matibabu na hali zao sio mbaya, wakati dereva wa gari T.542 DMS/680 DKS aina ya Howo ,anashikiliwa chini ya ulinzi wa polisi kituo cha afya Chalinze.

Chanzo cha ajali ni dereva huyo ambae anadaiwa alijaribu kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhali na kugongana uso kwa uso na gari T.504 DLV/904 DMN aina ya DAF.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

Habari Mchanganyiko

Yara yaja na bima ya mazao kwa wakulima

Spread the love  WAKATI serikali ikiweka mikakati mbalimbali kuimarisha sekta ya kilimo...

error: Content is protected !!