Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Wawekezaji watoroka na mabilioni 
Habari Mchanganyiko

Wawekezaji watoroka na mabilioni 

Noti za Elfu Kumi
Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), inawasaka wamiliki wa Kampuni ya MEIS Industies kwa tuhuma za kutoroka na fedha za kujenga kiwanda cha saruji mkoani Lindi, kiasi cha Sh. 46 Bilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 18 Juni 2019 na Takukuru, imewataja wamiliki hao kuwa ni Islam Ally Saleh, Merey Ally Saleh, Sabri Ameir Kuleib na Abdallah Said Abdallah Bin Aliya.

Taarifa ya Takukuru inaeleza kwamba, Kampuni ya MEIS ilikabidhiwa fedha hizo kama mkopo mwaka 2011 na Serikali ya Libya, ambazo zilikuwa sehemu ya fedha za uwekezaji zilizotolewa na taifa hilo kwa serikali ya Tanzania.

Lakini, uchunguzi wa taasisi hiyo umebaini kwamba sehemu kubwa ya fedha hizo walizokopeshwa kampuni ya MEIS zimetumika kwa matumizi mengine kinyume na makusudio ya serikali, jambo ambalo ni kosa chini ya Sheria ya Takukuru.

Taarifa hiyo imeeleza zaidi chimbuko la utolewaji wa fedha hizo, ikisema kwamba serikali ya Libya katika miaka ya 1980 iliikopesha  Tanzania mafuta ya Petrol na Diseli kiasi cha Metric tons 200,000. Ambapo kufikia mwaka 2005 nchi hiyo ilikuwa ikiidai serikali takribani Dola za marekani 200 Milioni.

Imeeleza kuwa, Serikali ya Libya ilisamehe nusu ya deni na zilizobakia ikakubaliana na Tanzania namna ya kulipa, ikiwemo Dola 61.0 Milioni zilipwe kwa mtindo wa madeni ya taifa, Dola za Marekani 20 Mil. zilipwe kwa mtindo wa DEPT SWAP, na dola 20.0 Mil. zifanye uwekezaji hapa nchini na baadae zirudishwe Libya na riba nafuu.

Kufuatia makubaliano hayo, mwaka 2009 serikali ya Libya na Tanzania zilisaini mkabata wa nyongeza ambao uliitaja kampuni ya MEIS kama kampuni itakayopewa kiasi cha dola 20.0 Milioni kwa ajili ya uwekezaji wa ujenzi wa kiwanda cha saruji eneo la Machore mkoani Lindi.

“Fedha hizo zilizotolewa kwa kampuni ya MEIS kama mkopo ambao ulipaswa kurejeshwa na riba nafuu na kwa mujibu wa mkataba, mkopo huo ulipaswa kurejeshwa ndani ya miaka 6 (2011 hadi 2017) hata hivyo, hadi kufikia mwaka 2019 kampuni ya MEIS haijarejesha mkopo na wala kiwanda cha saruji kilichokusudiwa kiujengwa hakijajengwa,” inaeleza taarifa ya Takukuru.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

error: Content is protected !!