Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wavulana 344 waliotekwa Nigeria waokolewa
Kimataifa

Wavulana 344 waliotekwa Nigeria waokolewa

Spread the love

BAADHI ya vijana wa kiume 344 waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram nchini Nigeria wameanza kuokolewa na vikosi vya usalama nchini humo. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Vijana hao wanadaiwa kutekwa wiki iliyopita kutoka shule ya bweni Kaskazini-Magharibi nchini Nigeria.

Msemaji wa Gavana wa jimbo la Katsina, Aminu Bello Masari amesema, wavulana waliokuwa wanashikiliwa katika Msitu wa Rugu wameachiliwa huru na wako katika hali nzuri.

Katika oparesheni ya uwokoaji, vikosi vya usalama kutoka nchini Nigeria, vilizingira eneo lote ambalo vijana hao walikua wamewekwa mateka na Boko Haramu na walipewa sheria ya kuto fyatua risasi.

Katsina amesema, vijana hao wamepelekwa katika jimbo la Katsina kufanyiwa uchunguzi wa kiafya kabla ya kureje katika familia zao.

Maafisa wa usalama na viongozi katika jimbo la Katsina wameeleza, kundi la Boko Haram liliagiza makundi matatu ya kihalifu kuwateka nyara mamia ya wanafunzi wa kiume kwa niaba yao.

Gavana wa jimbo hilo, Aminu Bello Masari alinukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema, “tumepata wavulana wengi. Sio wote,” huku chanzo cha usalama kililiambia shirika la habari la AFP wengine walibaki na watekaji wao.

Labaran alisema, hakuna hata mmoja wa wavulana waliotekwa nyara aliuawa, huku maoni yake yakikinzana na yale ya mvulana aliyeonyeshwa kwenye video hiyo ambaye alisema wengine waliuawa na ndege za kivita za Nigeria

Haijulikani jinsi kuachiliwa huru kwa wavulana hao kulitokea lakini habari hiyo imethibitishwa kwa BBC Hausa na afisa mwingine wa serikali ya jimbo hilo.

Uvamizi huo, ulifanywa na Awwalun Daudawa kiongozi wa genge moja la kialifu ambaye alipewa maagizo na Boko Haram, kiongozi huyo alishirikiana na viongozi wengine wawili wa magenge ya kihalifu.

Afisa mmoja wa Usalama nchini Nigeria amesema, Daudawa kama ”mnyang’anyi na mwizi wa ng’ombe kabla ya kuanza kutumia bunduki, akichukua silaha kutoka Libya ambako alipatiwa mafunzo na kuziuza kwa majambazi.”

Hata hivyo, zaidi ya wanafunzi 800 walikuwa shuleni wakati wa utekaji nyara, wengi wao walifanikiwa kutoroka katika eneo hilo na wengine kuingia mikononi mwa watekaji.

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amepongeza kikosi cha uwokoaji kwa kuwaokoa vijanua hao akisema ni ahueni kubwa kwa familia zao na nchi nzima, jamii na kimataifa kiujumla.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

Habari MchanganyikoKimataifa

Mgombea upinzani aongoza uchaguzi wa Rais Senegal

Spread the loveMgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameonekana kuongoza...

error: Content is protected !!